Jordan Riber

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jordan Riber ni mwongozaji, mtayarishaji na mwandishi wa miswada ya filamu wa Kitanzania mwenye asili ya Mzimbabwe.

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Riber alizaliwa katika familia ya son John na Louise Riber ambao wote ni wanafamilia katika mambo ya filamu; alikulia katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare na muda mwingi aliutumia katika kujifunza masuala ya utengenezaji wa filamu. Mwaka 2004 alimaliza masomo yake katika chuo cha Fairhaven College, nchini Marekani alikosomea mambo ya utayarishaji wa filamu.[1]

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2012, aliongoza tamthilia ya Siri ya Mtungi, iliyokuwa na nyota kama Cathryn Credo, Beatrice Taisamo, Yvonne Cherrie na wengine.[2] tamthilia ambayo ilichaguliwa kama tamthilia bora katika tuzo za 2014 Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA).[3]

Mwaka 2017 aliongoza filamu ya Hadithi za Kumekucha: Tunu.[4]

Mwaka 2018 aliongoza filamu nyingine ya Hadithi za Kumekucha:Fatuma aliyoitarisha na kuihariri yeye mwenyewe, ambao nyota wake walikuwa ni Cathryn Credo ,Beatrice Taisamo na Ayoub Bombwe.[5][6] Mwaka huohuo alitayarisha na kuongoza filamu ya Bahasha, iliyochezwa na Ayoub Bombwe, Godliver Gordian, Omary Mrisho na Cathryn Credo.[7][8][9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Out of Africa". Alumni WWU. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Siri Ya Mtungi". Worldcat. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. Colins, Charles (December 10, 2013). "Photos From Africa Magic @10 And AMVCA Nominee Announcement [KCee, Yvonne Okoro]". Gistmania. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "SGS Summer Film Festival: Hadithi Za Kumekucha: Tunu". Stanford University. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "Fatuma: Feature | Narrative". PAFF. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-09. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  6. "Fatuma". Chicago Reader. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. "Bahasha (2018)". IMDb. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. "BAHASHA". Toronto International Black Film Festival. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
  9. "Talent Factory: Catherin Credo". Dar es Salaam: Multichoice Africa. Iliwekwa mnamo November 10, 2020.  Check date values in: |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jordan Riber kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.