Nenda kwa yaliyomo

Betty Kazimbaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Taswira ya Mwanaidi (uhusika umechezwa na Betty Kazimbaya)

"Betty Aloyce Kazimbaya" (amezaliwa tar. 4 Machi, 1973[1]) ni jina la mwigizaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Anajulikana zaidi kwa kucheza uhusika wa Mwanaidi kutoka katika mfululizo wa televisheni maarufu wa Siri ya Mtungi (2012)[2].

Pia amecheza kama Mama Aisha (Samaki Mchangani—2014[3]), Mama Mwandenga (Going Bongo—2015), Mama Tumaini (Binti—2021[4]).

Mwaka wa 2021, amepata kuonekana katika tamthilia ya "Haikufuma" akicheza uhusika wa "Jalia."

Vilevile amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho Tanzania.[5]

Filamu alizocheza

[hariri | hariri chanzo]
Caption text
Na.Jina la filamuUhusikaMaelezo
1Neema1998—filamu ya kwanza
2Kijiweni2000
3Shangazi2002
4Wacha Masihara2012—2014, mchezo wa redio wa Hypermedia
5Siri ya MtungiMwanaidi2012
6Samaki MchanganiMama Aisha2014
7Going BongoMama Mwandenga2015
8BintiMama Tumaini2021
  1. "Betty Kazimbaya". IMDb. Iliwekwa mnamo 2021-08-26.
  2. Siri ya Mtungi (TV Series 2012) - IMDb (kwa American English), iliwekwa mnamo 2021-08-26
  3. Samaki Mchangani (Short 2014) - IMDb (kwa American English), iliwekwa mnamo 2021-08-26
  4. Binti (2021) - IMDb (kwa American English), iliwekwa mnamo 2021-08-26
  5. Going Bongo (2015) - IMDb (kwa American English), iliwekwa mnamo 2021-08-26