Amazonas (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha:Amazon near Manaus.jpg
Mto Amazonas karibu na Manaus
Mto wa Amazonas
Beseni ya Amazonas
Chanzo mlima Nevado Mismi (Peru)
Mdomo Atlantiki
Nchi Brazil (62.4%), Peru (16.3%)
Bolivia (12.0%), Kolombia (6.3%)
Ekuador (2.1%)
Urefu 6,400 km
Kimo cha chanzo takriban 5,597 m
Tawimito upande wa kulia Purus, Madeira, Tapajós, Xingu, Tocantins
Tawimito upande wa kushoto Marañón, Japurá, Rio Negro
Mkondo 219,000 m³/s
Eneo la beseni 6,915,000 km²
Miji mikubwa kando lake Manaus, Macapa, Santarem

Mto Amazonas (Kireno: Rio Amazonas) ni mto mkubwa duniani. Ina chanzo chake katika milima ya Andes inavuka beseni yake hadi Atlantiki kupitia eneo kubwa la misitu minene. Sehemu kubwa ya mwendo wake iko katika nchi ya Brazil. Inabeba maji zaidi kuliko mito ya Nile, Mississippi na Yangtse kwa pamoja.

Kuhusu urefu hakuna mapatano bado kama Nile au Amazonas ni mto mrefu duniani. Makadirio hutegemea ni tawimto upi mwenye chanzo cha mbali zaidi unaokubaliwa na wataalamu. 1969 urefu wake ulipimwa kuwa 6.400 km.[1]

Amazonas ina tawimito zaidi ya 10,000 na kati ya hizi kuna tawimito 17 zenye urefu wa zaidi ya 1,600 km zikishinda mito kama Senegal, Gambia au Nile ya buluu.

Upana wa mto ni wa kilomita kadhaa kufika hadi 100 km wakati wa mafuriko ya kila mwaka. Delta ya Amazonas ina upana wa mamia ya kilomita; ndani yake kuna kisiwa cha Marajó chenye eneo la 49,000 km² ambalo ni kubwa kushinda nchi kama Rwanda au Burundi.

Amazonas ni njia muhimu ya mawasiliano na usafiri nchini Brazil. Meli kubwa za baharini zinaweza kuingia hadi bandari ya Manaus iliyoko 800 km ndani ya bara. Meli ndogo za baharini hadi uzito wa tani 3,000 zinaweza kuvuka Brazil yote na kufika Peru.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
South America.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Amazonas (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.