Nenda kwa yaliyomo

Alois Beaulieu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alois Beaulieu, M.E.P. (Langon, Ufaransa, 8 Oktoba 1840 - Sai-Nam-Hte, 7 Machi 1866) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000. [1]

Padri huyo mmisionari alikatwa kichwa pamoja na askofu Simeoni-Fransisko Berneux na mapadri wawili wa shirika lake: Yusto Ranfer na Petro-Henri Dorie kwa sababu, walipoulizwa na watesi wamefika Korea kufanya nini, walijibu kwa ujasiri na unyofu kwamba wana lengo la kuokoa watu kwa jina la Yesu[2].

Hao na wafiadini wenzao 99 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[3]

Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba.

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Saint Louis Beaulieu". nominis.cef.fr. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92284
  3. "Korea and the church of martyrs". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-07.
  4. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
  5. The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.