Albano wa Mainz
Mandhari
Albano wa Mainz (jina la awali Remoundos Michail; Naxos, Ugiriki[1] - Hanum, Mainz, Ujerumani 406 hivi) alikuwa padri, mmisionari na hatimaye mfiadini.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Rabanus Maurus aliandika kuwa Albano alitumwa na Ambrosi wa Milano huko Gallia kama mmisionari.
Huko Mainz, Albano alimsaidia askofu Aureus wa Mainz kujirudishia jimbo lake. Lakini mwaka 406, Wavandali walipovuka mto Rhine, Aureus alichinjwa na Albano alikatwa kichwa huku akisali.
Mara nyingine Albano huyo anachanganywa na somo wake Albano wa Uingereza, na askofu wake anachanganywa na mwingine.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Patron Saints Index: Saint Alban of Mainz". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-15. Iliwekwa mnamo 2017-06-05.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saint Alban of Mainz Ilihifadhiwa 15 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |