Eneka : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
+kuongezea jambo |
||
Mstari 28: | Mstari 28: | ||
Lengo la Chibu kwa wimbo huu ilikuwa kupata ladha ya kimataifa na kusukuma gurudumu la Bongo Flava nje ya nchi. Alitoa nyimbo mbili kwa pamoja, [[I Miss You]] ukiwa Bongo Flava halisi huku Eneka ikiwa Afro-pop kwa ajili ya kimataifa.<ref>[https://www.nijuze.co.tz/burudani/eneka-ya-diamond-yampagawisha-yemi-alade/ Eneka ya Diamond yampagawisha Yemi Alade] Nijuze.com - July 12, 2017.</ref> |
Lengo la Chibu kwa wimbo huu ilikuwa kupata ladha ya kimataifa na kusukuma gurudumu la Bongo Flava nje ya nchi. Alitoa nyimbo mbili kwa pamoja, [[I Miss You]] ukiwa Bongo Flava halisi huku Eneka ikiwa Afro-pop kwa ajili ya kimataifa.<ref>[https://www.nijuze.co.tz/burudani/eneka-ya-diamond-yampagawisha-yemi-alade/ Eneka ya Diamond yampagawisha Yemi Alade] Nijuze.com - July 12, 2017.</ref> |
||
Huu ndio wimbo wa kwanza kwa Chibu kufanya kazi na mwongozaji Sesan kutoka Nigeria. Video ilifanywa nchini [[Afrika Kusini]].<ref>[http://topnaija.ng/video-diamond-platnumz-eneka-dir-sesan/ Video: Diamond Platnumz – Eneka (Dir. By Sesan)] TopNaija, July 13, 2017.</ref> |
|||
==Tazama pia== |
==Tazama pia== |
Pitio la 08:10, 4 Juni 2018
“Eneka” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kava ya Eneka
| |||||
Single ya Diamond Platnumz kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale | |||||
Imetolewa | 10 Julai, 2017 | ||||
Muundo | Upakuzi wa mtandaoni | ||||
Imerekodiwa | 2017 | ||||
Aina | Bongo Flava, Afro-pop | ||||
Urefu | 3:34 | ||||
Studio | Wasafi Records | ||||
Mtunzi | Diamond Platnumz | ||||
Mtayarishaji | Laizer Classic | ||||
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz | |||||
|
"Eneka" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 10 Julai, 2017 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz. Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa sita kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo. Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic kupitia studio za Wasafi Records. Awali baada ya kutoka, kulivuma taarifa ya kwamba mapigo ya wimbo yanafanana sana na wa Davido "Fall" uliotoka kabla ya Eneka.
Kwa taarifa hizo, mtayarishaji wa wimbo huu "Laizer Classic" alilamizika kutetea hoja hii kwa kupitia mtandao wa Millard Ayo na kusema: "Sioni ajabu kwamba mtu akisema hii imefanana…mi ninachojali ni kwamba watu watapokeaje nyimbo, itapendwa au itafanya vizuri. Hicho ndicho ninachokiangalia zaidi." Katika mahojiano, Laizer alikiri kama sehemu kubwa ya utengenezaji wa nyimbo hufuata mtindo wa Kinegeria na wao walitangulia hivyo lazima utafanana na wao.[1]
Lengo la Chibu kwa wimbo huu ilikuwa kupata ladha ya kimataifa na kusukuma gurudumu la Bongo Flava nje ya nchi. Alitoa nyimbo mbili kwa pamoja, I Miss You ukiwa Bongo Flava halisi huku Eneka ikiwa Afro-pop kwa ajili ya kimataifa.[2]
Huu ndio wimbo wa kwanza kwa Chibu kufanya kazi na mwongozaji Sesan kutoka Nigeria. Video ilifanywa nchini Afrika Kusini.[3]
Tazama pia
Marejeo
- ↑ Habari mpya kuhusu Eneka ya Diamond Platnumz kufanana na Fall ya Davido Eneka katika wavuti ya Millard Ayo, July 22, 2017.
- ↑ Eneka ya Diamond yampagawisha Yemi Alade Nijuze.com - July 12, 2017.
- ↑ Video: Diamond Platnumz – Eneka (Dir. By Sesan) TopNaija, July 13, 2017.