Maximilian Kolbe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Karatasi ya maombezi yenye mchoro wa Mtakatifu Maximilian Kolbe akimuomba Bikira Maria Imakulata huku amefungwa katika kambi la Wanazi.

Maximilian Maria Kolbe (8 Januari 189414 Agosti 1941) alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka nchi ya Poland.

Katika historia ya Kanisa anajulikana kwa jinsi allivyomheshimu Bikira Maria kwa jina la Imakulata, yaani Mkingiwa dhambi asili.

Baada ya kuanzisha chama cha Mashujaa wa Imakulata huko Roma (Italia) na Mji wa Imakulata huko Polandi, alikwenda Japani kama mmisionari.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alifungwa na wafuasi wa Unazi katika kambi ya wafungwa wa siasa kule Auschwitz. Hatimaye alijitolea kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila ya chakula hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili kifo kwa tumaini la Kikristo na bila ya chuki, na alipobaki peke yake aliuawa kwa sindano ya sumu.

Mwaka 1982 alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 14 Agosti kila mwaka[1].

Sala yake[hariri | hariri chanzo]

Wewe umenipenda milele, tangu u Mungu; hivyo umenipenda na utanipenda milele!...

Upendo wako kwangu ulikuwepo hata kabla sijakuwepo, na ni kwa sababu ya kunipenda, Mungu mwema, kwamba umeniita kutoka utovu wa vyote nianze kuwepo!

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • B. HANLEY, O.F.M., Maximilian Kolbe, Upendo uliokithiri – tafsiri ya Parokia la Mt. Maksimilian Kolbe, Mwenge, Dar-es-Salaam – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1992
  • Rees, Laurence. Auschwitz: A New History, Public Affairs, 2005. ISBN 1-58648-357-9

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.