Lugha ya kidini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Lugha ya kidini ni lugha inayotumiwa pekee katika maisha ya kidini kama vile kwa shughuli za litujia, sala au maandiko matakatifu wakati wasemaji au wasomaji wa lugha hii ya kidini hutumia lugha nyingine katika maisha ya kawaida.

Lugha za kale kama lugha za kidini[hariri | hariri chanzo]

Mara nyingi lugha za kidini ni lugha za kale zinazohifadhiwa katika maisha ya kidini lakini katika maisha ya kawaida zimeshabadilika sana.

Mfano wake ni Kislavoni cha Kanisani kilichokuwa lugha ya kawaida ya makabila ya Kislavoni mnamo mwaka 800 BK wakati akina Methodio na Kyrilo wa Saloniki walipotafsiri vitabu vya kikristo kwa ajili ya misioni ya Waslavoni. Lakini lahaja mbalimbali za Kislavoni zimeendelea kubadilika na lugha mpya za kislavoni zimetokea kama vile Kirusi, Kibulgaria n.k.. Tangu karne nyingi hakuna mtu anayetumia Kislavoni cha Kanisani kwa maisha ya kila siku lakini inaendelea kuwa lugha ya ibada na liturgia katika makanisa ya Kiorthodoksi ya mataifa ya Kislavoni kama vile vya Warusi, Wabulgaria, au Waserbia.

Mfano mwingine ni Kisanskrit kilichokuwa lugha ya Waaria walioingia Uhindi takriban miaka 1,500 KK kikawa lugha ya maandiko matakatifu. Kisanskrit hufundishwa hadi leo lakini lugha za leo zimekuwa tofauti kabisa.

Lugha za kidini zisizotumiwa tena katika maisha ya kila siku[hariri | hariri chanzo]

Lugha za kidini zinazoendelea kuzungumzwa au zilizo karibu na lugha hai[hariri | hariri chanzo]

Kuna pia lugha hai zinazotumiwa kama lugha za kidini nje ya eneo wanapokaa wasemaji wao. Mara nyingi hata katika lugha hizi za kidini maneno na matamshi yasiyo kawaida tena hutunzwa.

Kiarabu na Uislamu[hariri | hariri chanzo]

Mfano wake mkuu ni Kiarabu kama lugha ya kidini kati ya Waislamu. Lugha ya Korani yenyewe haizungumzwi na Waarabu lakini inasikilizwa na kueleweka kwa Waarabu wengi. Sarufi yake bado ni ileile kama ya Kiarabu sanifu cha kisasa.

Lugha za Ulaya kama Kiingereza na Kijerumani zinatumiwa pia kipekee katika maisha ya kidini kutokana na tafsiri za Biblia zinazotunza maneno ya karne zilizopita zisizo kawaida tena katika maisha ya kila siku. Kwa Kiingereza ni hasa tafsiri ya Mfalme Yakobo (King James) na kwa Kijerumani ni tafsiri ya Martin Luther.

Tabia hizi zaonekana katika lugha na tamaduni nyingi.