Aleksander Mashuhuri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Aleksander Mashuhuri (Mkuu)
Mfalme wa Masedonia
Aleksander jinsi alivyomshambulia mfalme Dario wa Uajemi kwenye mapigano ya Issos(mozaiki ya Aleksander mjini Napoli, Italia)
Kusimikwa 336
Vyeo vingine Mkuu wa shirikisho la Wagiriki, Shahansha wa Uajemi, Farao wa Misri, Bwana wa Asia
.
Wake Roksana wa Baktria
Stateira wa Uajemi
Parysatis wa Uajemi
Nasaba Nasaba ya Masedonia
Baba Filipo II wa Masedonia
Mama Olimpia wa Epiros
AlexanderTheGreat Bust.jpg

Aleksander Mashuhuri (au Aleksanda Mkuu, kwa Kigiriki Μέγας Αλέξανδρος, inayoandikwa kwa alfabeti yetu Megas Aleksandros) aliishi tangu Julai 356 KK hadi tarehe 11 Juni 323 KK.

Mfalme wa Masedonia (336323 KK), anajulikana kama mmoja kati ya amiri jeshi waliofanikiwa kupita wote wengine katika historia ya dunia. Kabla hajafariki bado kijana aliteka sehemu kubwa ya dunia iliyojulikana na Wagiriki wa zamani zake, kuanzia Ulaya mashariki kusini hadi India na Misri.

Mitazamo juu yake[hariri | hariri chanzo]

Katika Deuterokanoni anatajwa na vitabu vya Wamakabayo kama mwanzilishi wa dola lililoeneza ustaarabu wa Kigiriki hata kuhatarisha imani ya Wayahudi na kuwadhulumu wakati wa mwandamizi wake Antioko Epifane wa Syria.

Katika kitabu cha Kizoroastria cha kipindi cha kati ya Uajemi kilichoitwa Arda Wiraz Nāmag Aleksander anajulikana kama “Aleksander aliyelaaniwa” kwa sababu alishinda milki ya Uajemi na aliangamiza mji mkuu wake ulioitwa Persepolis. Lakini katika habari za baadaye za Uajemi, mpaka Irani ya siku hizi, anaitwa Eskandar na hata alishangiliwa wakati Ukuta Mkuu wa Sadd-e Eskandar ulijengwa wakati wa Ufalme wa Parthia.

Pia anajulikana katika desturi za Mashariki ya Kati kama Dhul-Qarnayn kwa Kiarabu na Dul-Qarnayim kwa Kiyahudi na Kiaramu, yaani "mtu mwenye pembe mbili", huenda kwa sababu picha kwenye sarafu za wakati wa utawala wake ilimwonyesha kama anazo pembe mbili za kondoo dume za mungu Ammon wa Misri.

Jina lake kwa Kihindi ni Sikandar, neno ambalo ni sawa na “mtaalamu” au “mtu stadi.”

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aleksander Mashuhuri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.