Homer
Homeri (pia: Homer; Kigiriki: Ὅμηρος homeros) ni jina la mshairi mashuhuri kabisa wa Ugiriki ya Kale. Mashairi makubwa yanayosimulia vita ya Troya (Ilias) na misafara ya mfalme Odiseo yamehifadhiwa kama kazi zake.
Maswali juu yake [hariri]
Wataalamu wa leo hutofautiana kama Homeri alikuwa kweli mtungaji wa mashairri haya au kama ni sehemu za mashairi haya tu yaliyotungwa naye wakiamini ya kwamba kwa jumla ni masahiri ya kale yaliyowahi kuimbwa kablaye. Pia kuna wataalamu wanaouliza kama Homeri alikuwa mtu wa kihistoria au kama ni jina tu lililopakwa kwa mashairi haya.
Maisha [hariri]
Kufuatana na mapokeo ya kale Homeri alikuwa mshairi kipofu aliyeishi katika eneo la Ionia (Asia Ndogo) lililokaliwa na walowezi Wagiriki mnamo karne wa 8 KK. Miji mbalimbali ya Ionia hutajwa kama mahali pa kuzaliwa kwake. Jina la mamake lilikuwa Kreitheïs. Anasemekana alikufa kwenye kisiwa cha Ios.
| Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Homer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |