Michezo ya Olimpiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bendera ya Olimpiki yaonyesha pete tano


Michezo ya Olimpiki ni mashindano ya michezo makubwa duniani inayofanyika kila baada ya miaka minne.

Michezo ya Olimpiki imekuwa na historia ndefu katika vipindi viwili:

  • Michezo ya Olimpiki ya Kisasa ya kwanza ilitokea mwaka 1896 mjini Athens (Ugiriki). Mwanzishilishaji alikuwa Mfaransa Pierre de Coubertin alitaka kutumia kielelezo cha michezo ya kale kwa kujenga uhusiano mzuri kati ya vijana wa nchi mbalimbali na kuwapatia nafasi ya kushindana kwenye uwanja wa michezo badala ya uwanja wa vita. Coubertin alianzisha Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (International Olympic Committee - IOC).

Michezo hii ya kisasa imeendelea kila baada ya miaka minne isipokuwa 1916, 1940 na 1944 kwa sababu ya Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia.

Michezo ya kisasa hufanyika katika mji mwingine kila safari. Michezo ya 2004 ilifanyika Athens, ya 2008 huko Beijing na ya 2012 itafanyika London.

Kuna tofauti kati ya michezo ya kiangazi na michezo ya majira ya baridi.

Washindi watatu wa kwanza wa kila mashindano hupewa medali ya dhahabu, fedha au shabha.

Pete olimpiki[hariri | hariri chanzo]

Pete tano uza olimpiki ni alama na nembo ya michezo tangu 1913. Pete tano zenye rangii tofauti humaanisha mabara matano.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]