Mozaiki
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mozaiki (mosaiki; ) ni mtindo wa pekee wa uchoraji picha unaotumia vipande vidogo vya kioo cha rangi au vigae vya rangi mbalimbali vinavyounganishwa kuwa picha. Kunawezekana pia kutumia vipande vya vitu vyovyote vyenye rangi vinavyoweza kuunganishwa kuwa picha.
Yaliyomo |
[hariri] Chanzo cha mtindo wa mozaiki
Mtindo huu ulionekana mara ya kwanza huko Phrygia (katika Uturuki ya leo) iliyokuwa sehemu ya ustaarabu wa Ugiriki ya Kale. Mawe ya rangi nyeupe na nyeusi yalipangwa ukutani au kwneye sakafu kuwa tarakibu.
Baadaye Wagiriki na zaidi Waroma waliendelea kuongeza rangi na kutunga picha kamili si tarakibu tu kwenye kuta za nyumba. Maghofu ya Kiroma yanaonyesha mifano mingi iliyodumu hadi leo.
[hariri] Mozaiki za Bizanti na za Waarabu
Sanaa ya mozaiki iliendelezwa katika ustaarabu wa Bizanti. Wabizanti walipamba makanisa, majumba ya kifalme na pia nyumba za matajiri kwa mozaiki nzuri kabisa.
Waarabu Waislamu walipotwaa shemu kubwa za milki ya Bizanti waliendelea kuwaajiri wasanii Wabizanti wakipamba misikiti kama msikiti wa Umawiya huko Dameski au majumba ya masultani.
Baadaye walikuwa mafundi Waislamu waliopamba makanisa na nyumba katika Italia ya kusini.
[hariri] Mozaiki leo
Mtindo wa mozaiki umeaendelea kutumiwa hadi leo. Kwa kawaida mozaiki inaendelea kuwa picha inayounganishwa kwa njia ya kudumu na ukuta au safau ya jengo fulani. Inawezekana pia kuifunga katika fremu na kubadilisha mahali pake lakini picha za mozaiki huwa nzito.
[hariri] Mifano ya mozaiki
|
Alexander Mkuu kwenye mapigano ya Issos, kigiriki, karne ya 1 KK |
Mozaiki ya kibizanti ya karne ya 6: Mamajuzi wakimtembelea mtoto Yesu; Kanisa la Sant'Apollinare Nuovo mjini Ravenna |
Mozaiki ya Kristo katika kanisa la Hagia Sophia mjini Istanbul |
|
|
Karne ya 19, Ujerumani (Braunschweig) |
Mozaiki ya Art Deco kwenye ukuta wa nje wa nyumba ya Nancy, Ufaransa |
Mozaiki inayoonyesha picha ya Pablo Picasso |
[hariri] Viungo vya Nje
- History of mosaics & custom mosaics gallery
- Society of American Mosaic Artists
- British Association for Modern Mosaic
- Mosaic art glossary - terms, definitions & images
- Mosaics resource
- Mosaic design tutorial
- Photos of mosaics in Hagia Sophia, Constantinople