Ziwa Timsah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ziwa Timsah (pia linajulikana kama Ziwa Mamba) ni ziwa lililopo nchini Misri katika Delta la Mto Nile. Linapatikana katika eneo la kuanzia Bahari ya Mediteranea hadi katika Ghuba ya Suez, kupitia katika kanda ya Maziwa ya Bitter.[1]

Mwaka wa 1800, mafuriko yalijaza eneo la Wadi Tumilat na kusababisha pande za ziwa Timsah kujaa na kufurika na hii ikasababisha kupeleka maji upande wa kusini kwenye Ziwa Bitter kiasi cha umbali wa maili tisa.[2] Mwaka 1862, ziwa hili lilifurika maji kutoka Bahari ya Shamu.[3]

Mfereji wa Suez, ambao ndio unaopeleka maji baridi katika eneo hilo, unakatiza katika ziwa Timsah. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maji, mfereji huo umepanuliwa na hivyo kusababisha kushuka kwa kina cha maji katika Ziwa Timsah. Hali hii iligunduliwa mwaka 1871.[4]

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ziwa Timsah lipo kati ya eneo la shingo ya nchi baina ya Bahari ya Shamu na Bahari ya Mediteranea.[5]

Kituo cha mwisho katika mteremko huo kuna maziwa yenye maji baridi ambapo ziwa Timsah ni moja kati ya maziwa hayo. Eneo la Ziwa Timsah ni kiasi cha maili za mraba 5.4.[6] Eneo kubwa la ziwa ni kina kirefu chenye tope lenye kimo cha futi 3 (mita 1).[7]

Imekwisha hakikishwa katika historia ya zamani ya Misri, kwamba Ziwa Timsah lilikuwa upande wa kaskazini, jirani na Bahari ya Shamu.[8][9]

Tarehe 4 Machi 1963, jiji la Ismailia, lililipata jina la ziwa hilo kutokana na makamu Ismail Pasha, kutokezea katika upande wa kaskazini wa mfereji. [10] Pia kuna pwani mbalimbali pembezoni mwa ziwa hili ikiwa ni pamoja na Moslem Youth, Fayrouz, Melaha, Bahary, Taawen, na pia kuna fukwe mbalimbali zinazomilikiwa na mamlaka ya Mfereji wa Suez.[11]

Mifereji[hariri | hariri chanzo]

Mfereji wa Suez katika Ismailia upande wa kaskazini mwa ukingo wa Mto Timsah, mwaka 1860 hivi. Umalizikaji wa ujenzi wa kuyaleta maji kutoka Ziwa Manzaleh kuja Mto Timsah.

Kuna uwezekano kuwa, ziwa Timsah lilikuwa lipo na limetumika kama kiungio katika utengenezaji wa mfereji wa Suez na hii inamaanisha kuwa ziwa hili lilikuwepo kiasi cha miaka 4,000 iliyopita, hususani katika kipindi cha kati cha utawala wa Misri,[12] na ulipanuliwa na Darius I.[13]

Ujenzi wa mfereji wa Suez ulianza jirani na ziwa Timsah mwaka 1861 na katika kipande cha kaskazini mwa ziwa hili.[14] Mwanzoni mwa ujenzi huu, maandalizi yalikuwa ni pamoja na kujenga nyumba kwa ajili ya wafanyakazi 10,000 na vyumba kwa ajili ya kuweka vifaa mbalimbali vya ujenzi.[14] 3,000 laborers dug a channel from the Nile to Lake Timsah in 1861 and 1862, which brought a fresh water supply to the area.[14][15] Pia ilipendekezwa kujenga bandari ndogo katika kilele kikiwa pamoja na mfereji.[16]

Sehemu ya eneo la Ismailia ya mfareji wa Suez, ambao umeunganika na Ziwa Manzala hadi ziwa Timsah, ulimalizika kujengwa Mwezi Novemba mwaka 1862. Matengenezo ya sehemu hiyo yalimalizwa na wafanyakazi wa lazima, ambao waliongeza nguvu kazi kiasi cha watu 8,000. Kazi ilianza upande wa kusini wa Ziwa Timsah kati ya mwaka 1862-1863, na upanuzi ukaendelea kuelekea kaskazini. Wafanyakazi wasio wa hiari walikuwa wakitumika wakati wa ujenzi huo, kuanzia mwezi Machi mwaka 1862, hadi Ismail Pasha alipoondoa sheria hiyo mwaka 1864. Kutokana na kujengwa mfereji huo, maji kutoka katika ziwa Manzaleh yalitiririka na kuingia katika ziwa Timsah. Upanuzi ukaendelea upande wa kaskazini hadi mwaka 1867, na sehemu ya kusini hadi mwaka 1876.

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Ziwa Timsah ni ziwa lenye asili ya weusi na pia hupata rutuba katika vipindi tofautitofauti. Kazi za binadamu katika ziwa hili zimesababisha athari mbalimbali, hasa kushuka kwa kiwango cha uzalishaji wake. Kupungua kwa rutuba katika ziwa hili kulianza kuonekana tangu mwaka 1871, hii ikiwa ni kufuatia na kujengwa kwa mfereji wa Suez na hatimaye kueongezwa kwa matawi kutoka katika mfereji huo kwenda katika matawi mbalimbali yanayohitaji..[7] The El-Gamil outlet serves as Lake Timsah's principal source of salt water.[7]

Chanzo pekee cha maji katika ziwa Timsah kilikuwa Mto Nile hadi lilipojengwa bwawa la Aswan na kuingilia mtiririko huu mwaka 1966, lakini pia maji kutoka chini ya ardhi pia huchangia kuweka maji katika ziwa hili.[7]

Mwaka 2003, makundi mbalimbali yalijaribu kupima kiwango cha uharibifu katika ziwa hili[17] na hii ilikuwa moja kati ya mambo muhimu zaidi kufanyika kutokana na umuhimu wa ziwa hili kwa wananchi wa maeneo ya ziwa hili.[17]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Gmirkin, Russell E. (2006). Berossus and Genesis, Manetho and Exodus. Continuum International Publishing Group, 231. ISBN 0567025926. 
 2. Hoffmeie, p.43
 3. Stanley, p.32
 4. Gollasch (2006). Bridging divides. Springer, 229. ISBN 1402050461. 
 5. Jerry R. Rogers, Glenn Owen (2004). Water Resources and Environmental History. ASCE Publications, 124. Retrieved on 2009-04-10. 
 6. Ismailia. Iliwekwa mnamo 2009-04-09.
 7. 7.0 7.1 7.2 7.3 Stephan Gollasch, Andrew N. Cohen (2006). Bridging Divides: Maritime Canals as Invasion Corridors. Springer, 229. Retrieved on 2009-04-10. 
 8. The Columbia Encyclopedia, Sixth Edition, s.v. "Suez Canal". Accessed 14 Mei 2008.
 9. Naville, Édouard. "Map of the Wadi Tumilat" (plate image), in The Store-City of Pithom and the Route of the Exodus (1885). London: Trubner and Company.
 10. Nourse, p.54
 11. Ismailia. Iliwekwa mnamo 2009-04-09.
 12. Shea, William H. "A Date for the Recently Discovered Eastern Canal of Egypt" Bulletin of the American Schools of Oriental Research, No. 226 (Apr., 1977), pp. 31-38
 13. Paice, Patricia "Persians" in Kathryn A. Bard and Steven Blake Shubert, eds. Encyclopedia of the Archeology of Ancient Egypt(New York: Routledge, 1999),
 14. 14.0 14.1 14.2 Royal Statistical Society (Great Britain), Statistical Society (Great Britain). (1887). Journal of the Royal Statistical Society. Royal Statistical Society, 503–509. Retrieved on 2009-04-10. 
 15. W.O. Henderson (2006). The Industrial Revolution on the Continent: Germany, France, Russia 1800-1914. W.O. Henderson, 151. Retrieved on 2009-04-10. 
 16. (2004) Water Resources and Environmental History. ASCE Publications, 124. ISBN 078440738X. 
 17. 17.0 17.1 Yasmine El-Rashidi. Making a city livable. Al-Ahram News. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-18. Iliwekwa mnamo 2009-04-09.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]