X Plastaz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
X Plastaz
Asili yake Arusha, Tanzania
Aina ya muziki Hip Hop
Miaka ya kazi 1996 - sasa
Studio Out Here Records


X Plastaz ni kundi la muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania lenye maskani yake jijini Arusha na lilianzishwa mwaka 1996. Ni miongoni mwa makundi maarufu sana katika anga ya muziki wa hip hop nchini Tanzania.[1]

Mtindo wao unachanganya vipengele vya muziki wa hip hop ya kimataifa na muziki wa asili wa Kimasai, unaowakilishwa na mwimbaji wa Kimasai Merege. Wakati Merege anaimba kwa maa (lugha ya Kimaasai), washiriki wengine wa kikundi wanarap kwa Kiswahili na kihaya. Merege pia anajulikana sana kwa kutumbuiza katika mavazi ya kitamaduni ya Kimasai. [2]

Nyimbo za X Plastaz kama vile Aha!, Dunia dudumizi, Bamiza na, hasa, Msimu kwa msimu ni miongoni mwa nyimbo maarufu zaidi katika muziki wa bongo fleva.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kundi la X Plastaz lilianzishwa na Nelson (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Father Nelly) na Godson Rutta (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Gsan) ndugu kutoka Arusha, pamoja na rafiki yao Ziggy kutoka Mkoa wa Tanga. [3]Walianza kujihusisha na hip hop mwaka wa 1995, wakiwa wanafanya kazi kwenye saluni ya kunyoa nywele.[4] Mnamo 1996 walitambuliwa na Bonnie Luv, mtayarishaji wa muziki kutoka Dar es Salaam, ambaye aliwafanya warekodi wimbo mmoja. Wimbo wao wa kwanza ulikuwa Bamiza (1998), ilikuwa moja ya nyimbo zilizochezwa sana na redio za Tanzania kwa wiki kadhaa. Wimbo mwingine ulifuata punde, Wachaga piga chata.

Mwaka 1997, X Plastaz walitembelea kijiji cha kimaasai magharibi mwa Arusha na kukutana na Yamat Ole Meipuko, pia anajulikana kama Merege, [5]ambaye alikuwa mshindi wa mashindano mbalimbali ya uimbaji wa Kimasai. Walimkaribisha Merege kujumuika nao walipokuwa wakitumbuiza katika maeneo ya Arusha na Moshi. Mtindo wao mpya wa "Hip hop ya Kimaasai" ulipata umaarufu sana, Merege aliongeza kipengele cha kipekee kwenye muziki wao. Baada ya muda, kundi lilipata wanachama wapya, ambao ni wadogo wa Ruff na Gsan (wa kike alikua na miaka 13 na na wa kiume miaka 11).[6]

Mnamo Novemba 2002, X Plastaz walitumbuiza nchini Uholanzi katika tamasha la kimataifa la Siku ya UKIMWI Duniani. Mnamo Julai 2003, wakati wa ziara yao barani Ulaya, X Plastaz walitumbuiza kwenye Couleur Cafe Festival (Brussels), Rita Ray’s the Shrine night (London)[7] na Respect Festival iliyofanyika Millennium Dome jijini London.[8] Muziki wa X Plastaz ulimvutia Jay Rutledge, mhariri wa mfululizo wa CD za Rough Guides ethnic music, wimbo wao wa 'Msimu kwa Msimu' ulijumuishwa kwenye albamu ya mkusanyiko ya 'Rough Guide to African Rap'.

Mwaka wa 2004, kampuni ya Kijerumani ya kurekodi muziki ya Out Here Records ilitoa albamu ya kwanza ya X Plastaz, Maasai Hip Hop, ambayo ilijumuisha nyimbo maarufu zilizotolewa hapo awali katika Rough Guides.[9] Video za wimbo wa ‘Aha’ na ‘Ushanta’ zilichezwa mara kwa mara Channel O (Afrika Kusini). Mnamo 2005, X Plastaz walitumbuiza kwenye tamasha la PercPan huko Rio de Janeiro na Salvador (Brazil).[10]

Mnamo 2006, X Plastaz walipata kifo cha ghafla cha Father Nelly, alikufa kwa majeraha mnamo Machi 29 baada ya kuchomwa kisu. Alizaliwa mwaka wa 1976, alikuwa mwanachama mkongwe zaidi wa kundi na mtazamo wake wa huruma dhidi ya maskini na wahitaji ulikuwa mojawapo ya nembo za X Plastaz. Video ya wimbo wa mwisho wa Nelly, Nini dhambi kwa mwenye dhiki, ilirekodiwa kwenye mlima wa volcano wa Ol Doinyo Lengai, ni mojawapo ya video za muziki za Afrika maarufu kwenye YouTube. Licha ya kumpoteza mwanachama mkongwe, X Plastaz haikuvunjika, na bado inafanya kazi hadi leo. Mnamo 2009, walitoa Furaha, wimbo wa kwanza wa albamu yao ijayo. Sambamba na hilo, Gsan alishiriki katika BET Cypher, mkusanyiko wa kila mwaka wa wasanii wa Hip hop huko Brooklyn, New York. [11] Mnamo 2010, walitoa wimbo mwingine mpya, Afrika, katika tamasha la Sauti za Busara huko Stone Town, Zanzibar.[12][13]

X Plastaz na utamaduni wa Kitanzania[hariri | hariri chanzo]

Kando na kujumuisha sauti za Wamasai katika nyimbo zao, X Plastaz huegemeza taswira yao kwenye utamaduni wa Kimaasai kwa hadhira ya Tanzania na kimataifa. Moja ya nyimbo zao maarufu, Aha!, inahusu maisha ya kijiji cha kimaasai, na video ya wimbo huu ilirekodiwa katika kijiji cha kitamaduni, ikionyesha mtindo wa maisha na desturi za Wamasai. Rapu ya wimbo huo ni ya kiswahili na kihaya, wakati kiitikio ni wimbo wa kimaasai. Wimbo huu pia ulijumuishwa katika filamu ya HBO This Is My Africa.[14]

Kama ilivyo kawaida kwa wanamuziki wengi wa hip hop, mashairi ya X Plastaz mara nyingi yanahusu masuala ya kijamii na kisiasa. Kupitia nyimbo zao, X Plastaz huvuta hisia za wasikilizaji kwenye matatizo makubwa ya Tanzania na Afrika kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na umaskini, UKIMWI, na vita.[15]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

  • Maasai Hip Hop (Out Here Records 2004). Orodha ya nyimbo: "Dunia dudumizi", "Bamiza", "Kitita", "Shika Iako", "Nini Dhambi kwa mwenye dhiki?", "Msimu kwa msimu", "Wachaga piga chata","Ushanta", "Kutesa kwa zamu", "Aha!", "Kusanyikeni", "Haleluya", "Not Ready"[16]

References[hariri | hariri chanzo]

  1. "X Plastaz biography". Last.fm (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  2. Thompson, K. D. (2008). Keeping It Real: Reality and Representation in Maasai Hip-Hop. Journal of African Cultural Studies, 20(1), 33–44. http://www.jstor.org/stable/25473396
  3. "African Rappers Speak | Arts | The Harvard Crimson". www.thecrimson.com. Iliwekwa mnamo 2022-06-09. 
  4. "AfricaUnsigned.com - X Plastaz". web.archive.org. 2010-12-12. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-12. Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  5. "X Plastaz". Discogs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  6. "AfricaUnsigned.com - X Plastaz". web.archive.org. 2010-12-12. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-12. Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  7. "Rita Ray". the Guardian (kwa Kiingereza). 2003-02-28. Iliwekwa mnamo 2022-06-09. 
  8. "X PLASTAZ | Out | here records" (kwa de-DE). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-07. Iliwekwa mnamo 2022-06-09. 
  9. "X PLASTAZ – Maasai HipHop | Out | here records" (kwa de-DE). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-07. Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  10. "PercPan começa hoje com ingressos esgotados - Cultura". Estadão (kwa pt-BR). Iliwekwa mnamo 2022-06-09. 
  11. "Tanzanian emcee in BET Hip Hop Awards cypher". Africanhiphop (kwa en-US). 2009-10-26. Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  12. "X Plastaz at Sauti za Busara 2010 | XPS". web.archive.org. 2011-07-15. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-15. Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  13. "X Plastaz launching new video ‘Africa’ featuring Fid Q & Bamba Nazar". Africanhiphop (kwa en-US). 2011-10-27. Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  14. "AfricaUnsigned.com - X Plastaz". web.archive.org. 2010-12-12. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-12. Iliwekwa mnamo 2022-06-07. 
  15. Lemelle, Sidney J., Ni wapi Tunakwenda: Hip Hop Culture and the Children of Arusha. In The Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres
  16. "Maasai Hip Hop" at iTunes