Channel O

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Channel O

Channel O ni kituo cha muziki chenye makao yake Afrika Kusini ambayo ilianza kupeperusha vipindi kwa mara ya kwanza mapema katika miaka ya tisini. Wazo lake kuu ni muziki wa Kiafrika barani Afrika na ng'ambo. Katika miaka iliyopita, stesheni hii ya muziki imefanya majina ya watangazaji wake kujulikana sana kama vile Mimi, Nonhle, KB, Miss Candy.

Channel O inaweza kupatikana kupitia DSTV, hudumua ya Runinga ya kulipia kwa wakaazi takriban wote barani Afrika. Stesheni hii hupeperusha vipindi mbalimbali vya muziki kama vile Kwaito, Mbhaqanga , Injili (kutoka Afrika na ya Kimataifa), Hip hop, na mingine mingi. Huonyeshwa pia asubuhi katika Magicworld.

Pia huandaa mashindano ya kila mwaka ya Channel O Music Video Awards sherehe ambapo wasanii hutuzwa kwa mchango wao bora kwa muziki.

Mapokezi[hariri | hariri chanzo]

Channel O inajulikana kwa vipindi vyake vyenye uwezo wa mapokezi na majibizano, hasa O-Boma, na baadaye Oboma Express na Young, Gifted and African. Wakati wa wikendi pia hupeperusha kipindi kingine, The 411 ambapo unaweza kujiona na ujumbe wako kwenye Runinga. Kiko na kuta za video na watazamaji ndio wanaochagua orodha ya nyimbo zitakazochezwa.

Kuta za Video[hariri | hariri chanzo]

Kutz ya video iliyo kuu zaidi ni O Express (kwa asilia Hit Train). Kuta nyingine ni za miziki maalumu kama vile: pop, Rock, RnB, Injili, Wadada pekee, Wafalme na pia x vs x ambapo video za waimbaji wawili huonyesha katika saa moja. Ina kuta ya video ukuta bila mapumziko ya matangazo ya biashara inayoitwa Heatwave ambayo hupeperushwa kati ya 1500-1600 kila siku. Pia kuna kuta kwa watazamaji kuchagua na pia orodha ya miziki bora kutoka chini hadi juu. Kabla ya tuzo za Channel O zinapofanyika, miziki iliyoteuliwa huchezwa tu katika kuta.

Lelo[hariri | hariri chanzo]

Hapa ndipo video za muziki huchanganywa. DJ huchanganya nyimbo hasa kwa ajili ya kipindi hicho. Ni maarufu sana na toleo jipya linalopeperushwa linaitwa Lower Level only fresh music.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]