Nenda kwa yaliyomo

William Wallace

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya William Wallace, Aberdeen, Uskoti.

William Wallace alikuwa askari wa Uskoti ambaye alipigana na Mfalme wa Uingereza Edward I kwenye Karne za kati. Alizaliwa mnamo 1272, akanyongwa na Waingereza tarehe 23 Agosti 1305. Scotland ilikuwa inadaiwa na Edward, ambapo Wallace akakataa kumtii Edward.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wallace alizaliwa kati ya miaka 1270-1272. Ni vitu vichache tu vinavyofahamika kuhusu kuzaliwa kwake au utoto wake. Mahali husika pamoja na muda ambao Wallace alizaliwa bado havijafahamika vizuri mpaka sasa. Watu wengine husema kuwa alizaliwa mnamo mwaka 1272, lakini kitabu kilichochapishwa kwenye karne ya 16 kiitwacho History of William Wallace and Scottish Affairs kinasema alizaliwa mwaka 1276. Jamii ilisema alizaliwa Elderslie, karibu na Paisley uliopo Renfrewshire. Kuna viungo katika Ayrshire pia, na bado pia haipo wazi kuwa Wallace alipigana na Waingereza wa Ayrshire au Lanark.[1][2][3] Jamii ilimwona Wallace kama mtu wa kawaida tu. Robert the Bruce, ambaye pia alipigana na Waingereza, alionekana kuwa mtu mwenye heshima. Lakini huu si ukweli madhubuti kwa sababu familia ya Wallace ilikuwa na heshima kwa kiwango fulani pia.

Mapambano

[hariri | hariri chanzo]

Mfalme Edward aliwapa Waskoti mpango uliowawezesha kuwa na mfalme wa Kiskoti kwa muda mrefu, huku Mfalme Edward akiwa bado msimamizi. Hii iliwafanya Waskoti kutoa heshima kwa kupiga magoti, na kuapa kwa utii kwake kwa hiari yao. Wallace alikataa, na kuongoza upinzani kumfuata. Kulikuwa na mfululizo wa vita vilivyopigwa:

Baada ya jaribio, tarehe 23 Agosti 1305, Wallace alichukuliwa kutoka ukumbini, wakamvua nguo na kumvuta mpaka mjini kwenye visigino vya farasi mpaka Elms iliyopo Smithfield. Alinyongwa, na kupewa hukumu mojawapo ya kutisha kuwahi kutokea Uingereza katika sheria zao. Ilimaanisha kuwa alinyongwa lakini aliachiliwa akiwa bado hai, mwili wake ulikatwakatwa na utumbo wake kuchomwa moto. Baadaye akakatwa kichwa na mwili wake kukatwa katika vipande vinne. Kichwa chake kilihifadhiwa kwenye lami.[4] Na baadaye kuwewekwa pamoja na vichwa vya kaka zake John na Simon Fraser, ambao walikua wafuasi wake. Viungo vya Wallace vilionyeshwa tofautitofauti, katika Newcastle upon Tyne, Berwick-upon-Tweed, Stirling, and Aberdeen.

Kumbukumbu

[hariri | hariri chanzo]

Kitabu cha The Acts and Deeds of Sir William Wallace, Knight of Elderslie kilichoandikwa na mpigakinanda Blind Harry mnamo karne ya 15. Kitabu hiki kiliandikwa kama hadithi kuliko toleo la kweli la maisha yake, na kuchangia kuwepo kwa wakongwe wakubwa kama William Wallace. Filamu iitwayo Braveheart inalingana na riwaya.

Ubao wa matangazo uliopo katika ukuta wa St Bartholomew's Hospital karibu na eneo walilomhukumia Wallace lililopo Smithfield.

Mwaka 2002 William Wallace alipewa nafasi ya 43 kati ya Mashujaa Waingereza wakubwa 100 kuwahi kutoa.[5]

  1. Emmons, Jim. "William Wallace." World History: Ancient and Medieval Eras. ABC-CLIO, 2013. Web. 27 Feb. 2013.
  2. World History: Ancient and Medieval Eras Feb. 27 2013
  3. Gillingham, John. "Wallace, Sir William." World Book Student. World Book, 2013. Web. 27 Feb. 2013.
  4. "The Trial Of William Wallace". Angelfire.com. Iliwekwa mnamo 2010-04-04.
  5. "100 Great British Heroes". BBC News. 2002-08-21. Iliwekwa mnamo 2010-04-04.