William Augustao Mgimwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

William Augustao Mgimwa (20 Januari 19501 Januari 2014) alikuwa mwanasiasa nchini Tanzania na mwanachama wa Chama cha Mapinduzi, aliyepata kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga kutokea mwaka 2010 hadi 2014; pia alikuwa waziri wa fedha kuanzia mwaka 2012 hadi 2014.[1]

Maisha ya Awali na Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Mgimwa alisoma katika seminari ya Mafinga na shule ya Tosamaganga, baadae alikuja kuijunga na chuo cha usimamizi wa fedha kiitwacho The Institute of Finance Management pamoja na Chuo Kikuu cha Mzumbe

Mgimwa alifanya kazi katika benki ya National Bank of Commerce (NBC) na mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge wa Kalenga kwa kura 31,421 na mnamo mwezi Mei 2012 rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alimteua kuwa waziri wa fedha.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Mgimwa alifariki tarehe 1 Januari mwaka 2014 akiwa nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Kloof Medi-Clinic ilioyopo katika jiji la Pretoria na kuzikwa siku ya Jumatatu ya tarehe 6 katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa.[2][3]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

RATIBA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA Archived 21 Januari 2022 at the Wayback Machine.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Member of Parliament CV". Parliament of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-02. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2012. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Finance Minister Dr Mgimwa dies in SA", 2 January 2014. 
  3. "Mgimwa dies in South Afric". The Citizen. 2 Januari 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-01. Iliwekwa mnamo 2 Januari 2014. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)