Nenda kwa yaliyomo

When You're Mad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“When You're Mad”
“When You're Mad” cover
Single ya Ne-Yo
kutoka katika albamu ya In My Own Words
Imetolewa Aprili 2006 (Marekani)
Muundo Digital download, CD single
Imerekodiwa 2005
Aina R&B
Urefu 3:43
Studio Def Jam
Mwenendo wa single za Ne-Yo
"So Sick"
(2006)
"When You're Mad"
(2006)
"Sexy Love"
(2006)

"When You're Mad" ni wimbo wa tatu kutoka katika albamu ya kwanza ya mwimbaji-mtunzi wa muziki wa R&B-pop wa Kimarekani Ne-Yo. Wimbo unatoka katika albamu ya In My Own Words. Wimbo ulipata kushika nafasi ya 15 katika chati za Billboard Hot 100 bora na kufikia hadi katika tano bora ya chati ya muziki wa R&B. Wimbo huu ni wa pili katika moja kati ya nyimbo za Ne-Yo ambazo hazikutolewa katika Uingereza.

Maelezo ya wimbo[hariri | hariri chanzo]

Wimbo unazungumzia jinsi Ne-Yo anavyoweza kuongea sana na wasichana wengine, kitendo ambacho kinamtia wazimu mno mpenzi aliyenaye. Ne-Yo aligundua pale mpenzi wake akiwa amekasirika anakuwa na mvuto wa ajabu, na anafanya vyovyote awezavyo ili aweze kumkera mpenzi wake huyo. Pale wale wote wakiwa na wazimu, halafu baadaye wanaonekana wakiwa wamelala pamoja, huku wakiwa wamesahau kile kilichowafanya wawe na wazimu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]