Lemuri-ukosi
Zana
Kijumla
Chapa/peleka nje
Miradi mingine
Mandhari
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Varecia)
Lemuri-ukosi | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Lemuri-ukosi mwekundu
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 2
|
Lemuri-ukosi (kutoka Kiingereza: ruffed lemur) ni spishi za lemuri wa jenasi Varecia katika familia Lemuridae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Jina lao linatoka kwa ukosi wa manyoya kuzunguka shingo yao. Rangi yao ni kahawianyekundu au nyepe na nyeusi. Spishi hizi ni lemuri wakubwa kuliko wote wengine wa familia hii (urefu wa mwili: sm 43-57, na uzito: kg 3-4). Hula matunda na mbochi, na husaidia kutawanya mbegu za miti.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Varecia rubra, Lemuri-ukosi Mwekundu (Red ruffed lemur)
- Varecia variegata, Lemuri-ukosi Mweupe-na-mweusi ( Black-and-white ruffed lemur)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Lemuri-ukosi mweupe-na-mweusi
-
Lemuri-ukosi mweupe-na-mweusi na mwekundu
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Lemuri-ukosi&oldid=994142"