Nenda kwa yaliyomo

Utenzi wa Gilgamesh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kibao cha udongo chenye Utenzi wa Gilgamesh kwa mwandiko wa kikabari.

Utenzi wa Gilgamesh ni shairi refu kutoka Mesopotamia ya Kale, ukiwa kati ya kazi za kwanza zinazojulikana za fasihi andishi duniani. Unasimulia habari za mfalme na nusu-mungu Gilgamesh na safari zake pamoja na rafiki yake Enkidu.

Utenzi huu unaaminiwa ulitungwa kati ya miaka 2400 KK na 1900 KK.

Unajulikana hasa kutokana na hadithi ya gharika kuu iliyofunika dunia yote ambayo hufanana na habari za Nuhu katika Biblia.

Mapokeo ya utenzi wa Gilgamesh

[hariri | hariri chanzo]

Utenzi huu haujulikani kwa sehemu zake zote. Ulisahauliwa mpaka ulipogunduliwa upya katika karne ya 19, wakati ambako wanaakiolojia walianza kusoma mwandiko wa kikabari uliosahauliwa kwa milenia mbili.

Toleo lililohifadhiwa vema ni vigae vya mwandiko wa kikabari 12 zilizotambuliwa katika mabaki ya mfalme Ashurbanipal (karne ya 7 KK). Maneno yake yamekamilishwa kutokana na matoleo mengine yaliyopatikana kwenye vibao vya udongo mahali pengine, ingawa mara nyingi ni vipande tu, si vibo kamili vilivyohifadhiwa kwa muda mrefu.

Wataalamu hufikiri ya kwamba hadithi mbalimbali juu ya mfalme Gilgamesh zilisimuliwa na kuandikwa tangu muda mrefu hadi zilipokusanywa katika utenzi mmoja kabla ya karne ya 7 KK.

Hadithi ya utenzi wa Gilgamesh

[hariri | hariri chanzo]

Mshujaa wa utenzi Gilgamesh ana tabia za mchanganyo, theluthi 1 yeye ni mwanadamu na theluthi 2 ni mungu. Ana nguvu kubwa sana lakini hana uhai wa milele. Anatawala mji wa Uruk. Mipango yake ya ujenzi na ukali wake zinasumbua raia wa Uruk.

Ombi la wakinamama wa Uruk

[hariri | hariri chanzo]

Hasa kawaida yake ya kudai usiku wa kwanza na bibiarusi kila safari ndoa mpya inatokea inasababisha wanawake wa mji kumwomba mungu Ishtar kuwasaidia. Ishtar anapeleka ombi kwa babake aliye mungu mkuu An anayemwamuru mungu mama Aruru kumwumba Enkidu kwa kutumia udongo. Kusudi ni kumpa Gilgamesh mwenzake aliye nguvu sawa naye na kwa njia hii kubadlisha tabia zake. Gilgamesh anaambiwa kwa njia ya ndoto ya mamake Ninsun ya kwamba Enkidu atakuja anamfurahia.

Enkidu anachukuliwa Uruk

[hariri | hariri chanzo]

Enkidu anaishi porini pamoja na wanyama witu anajisikia ni mmoja wao ana nywele nyingi kama mnyama. Mwindaji mmoja anatambua ya kwamba wanyama hawingii tena katika mitego yake kwa sababu wanalindwa na Enkidu. Anaenda Uruk na kulalamika mbele ya mfalme. Gilgamesh anamwambia kurudi pamoja na kahaba Shamhat; huyu Shamhat atamvuta kwa njia ya ngono kutoka upande wa kinyama kuja upande wa kibinadamu. Na kweli Enkidu anavutwa na Shamhat anafanya mapenzi naye kwa wiki moja. Katika muda huu wanyama pori wa Enkidu wanaondoka na kupotea. Enkidu anajikuta bila wanyama anaamua kumfuata Shamhat kwenda Uruk.

Enkidu apigana na simba; picha kwenye mhuri wa Kimesopotamia

Njiani wanakutana na wafugaji na katika kambi lao Enkidu anaonja mkate na bia mara ya kwanza. Kinyozi anaondoa nyewele za mwilini na kwa njia hii Enkidu anakuwa mwanadamu kamili.

Gilgamesh na Enkidu wanachukua miti ya mingati

[hariri | hariri chanzo]

Mjini Uruk Enkidu anakutana na Gilgamesh na wanaanza kupigana akiingia tena katika chumba cha bibi arusi. Nguvu zao zinalingana hakuna mshindi. Baada ya kuchoka wanapatana na kuwa marafiki. Wanapanga kwneda pamoja na kumwua Humbaba mlinzi wa msitu wa mingati ulio mali ya Ishtar. Mamake Gilgamesh anayeitwa Ninsun anaona hatari anamwomba mungu wa jua Shamash asaidie. Vilevile anampokea Enkidu kama mwanake hivyo huyu na Gilgamesh wamekuwa ndugu na wote wanapewa alama yake shingoni.

Akina kaka wawili wanafika msituni wanapigana na mlinzi Humbaba na kumwua kwa msaada wa Shamash. Wanakata miti na kujenga shapa halafu wanarudi kwa njia ya mto Frati wakibeba kichwa cha Humbaba.

Mapigano na ng'ombe dume wa mbinguni na kifo cha Enkidu

[hariri | hariri chanzo]

Ishtar anamwona Gilgamesha akirudi anampenda lakini anakataliwa. Akasirika juu yake na kwenda kwa babake mungu mkuu Anu anawomba umtuma ng'ombe dume wa mbinguni kama adhabu. Zimwi huyu akifika Uruka analeta hasara kubwa na kuua wanaume mamia. Enkidu na Gilgamesh wanaamua kupigana naye wanamshinda na kumchinja, moyo wake wanapeleka kama sadaka kwa Shamash. Ishtar akiona kifo chake analia lakini Enkidu anatupa mguu wa ng'ombe kwake.

Hapa miungu wa mbinguni wanaamua ya kwamba wote wawili wanastahili kifo lakini wanamteua Enkidu afe ingawa Shamash anawaombea. Enkidu anaona tishio hili katika ndoto. Anaanza kuwalaana miungu, anamlaana pia mwindaji na Shamhat waliomtoa porini. Shamash anajibu kutoka mbinguni akimkumbusha Enkidu jinsi gani Shamhat alimlisha na kumpa nguo anajaribu kumfariji kwa kumhakikisha ya kwamba atazikwa kwa heshima kubwa. Katika ndoto ya pili Enkidu anaona jinsi anavyopelekwa na malaika wa kifo kwenda ahera katika dunia ya wafu. Hapo gizani wakazi hula udongo wakivaa manyoa kama ndege na kuangaliwa na viumbe vya kutisha. Baada ya kuona haya yote Enkidu anakufa.

Matanga ya Gilgamesh na safari yake kutafuta masha ya milele

[hariri | hariri chanzo]

Kifo chake kinamsikitisha Gilgamesh anaondoka kwa matembezi marefu akitafuta siri ya maisha. Anaogopa kuadhibiwa sawa na Engidu kwa hiyo anatafuta ushauri wa babu yake Utnapishtim. Huyu na mkewe ni watu wa pekee wasiokufa katika gharika kuu iliyotumwa na miungu wakapewa maisha ya milele. Wanaishi kwenye kisiwa katika ziwa la mauti.

Gilgamesh anazunguka kote hadi anafika kwenye mlima Mashu penye mlango wa shimo la handaki linalopitiwa na jua Shamash kila usiku wakati asipoonekana. Gilgamesha anafaulu kupata kibali cha walinzi wa handaki apite. Akifika mwisho anainia katika bustani ya almasi anapoingia katika kilabu na kupata maelezo jinsi gani kumkuta Urshanabi anayeendesha feri ya kuvuka maji ya mauti. Anamkuta Urshanabi pamoja na viumbe vikubwa wanaomtisha hivyo anawaua. Hapa Urshanabi anamwambia ya kwamba aliua viumbe vya pekee vilivyoweza kumsaidia kuvuka kwa sababu wanatengeneza vijiti virefu vya jiwe ambavyo pekee vinaweza kutumiwa katika maji ya mauti.

Anamshauri Gilgamesh kukata miti 300 na kuchonga vijiti vya kusukuma feri. Kila baada ya kutumia kijiti Gilgamesha anakiacha kwenye maji maana imeshaharibika kwa kuingia katika maji ya mauti. Baada ya kumaliza vijiti 300 vyote bado hawakufika kisiwani lakini sasa wanatumia shati kama tanga. Haijulikani jinsi wanavyofik kwa sababu sehemu hii ya kibo cha udongo imepotea. Kisiwani Gilgamesha anamsimulia hadithi yake kwa mzee Utnapishtim. Huyu anamkataa na kumwambia hana budi kushiriki katika hali ya wanadamu wote haiwezekani kukimbia mauti.

Gilgamesh anamwuliza kwa nini yeye pamoja na mkewe wana maisha ya milele na hapa Utnapishtim anasimulia hadithi ya gharika kuu. Taarifa hii inafanana na habari za Biblia kuhusu Nuhu na kwa sababu hii Utnapishtim ameitwa pia "Nuhu wa Mesopotamia" na wataalamu wengine wanasema ya kwamba hadithi yake ilikuwa labda mfano kwa kutunga hadithi ya Nuhu.

Mwishoni Gilgamesh anarudi Uruk; mwisho wa masimulizi hauna uhakika kwa sababu ya mapengo katika maandishi.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jina la Gilgamesh linapatikana katika orodha ya wafalme wa Uruk: anaaminiwa alitawala katika kipindi cha kati ya 2700 KK na 2500 KK.

  • George, Andrew R., trans. & edit. (2003). The Babylonian Gilgamesh Epic: Critical Edition and Cuneiform Texts. England: Oxford University Press. ISBN 0-19-814922-0.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  • George, Andrew R., trans. & edit. (1999, reprinted with corrections 2003). The Epic of Gilgamesh. Penguin Books. ISBN 0-14-044919-1. {{cite book}}: Check date values in: |year= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  • Foster, Benjamin R., trans. & edit. (2001). The Epic of Gilgamesh. New York: W.W. Norton & Company. ISBN 0-393-97516-9.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  • Kovacs, Maureen Gallery, transl. with intro. (1985,1989). The Epic of Gilgamesh. Stanford University Press: Stanford, California. ISBN 0-8047-1711-7. {{cite book}}: Check date values in: |year= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) Glossary, Appendices, Appendix (Chapter XII=Tablet XII). A line-by-line translation (Chapters I-XI).
  • Jackson, Danny (1997). The Epic of Gilgamesh. Wauconda, IL: Bolchazy-Carducci Publishers. ISBN 0-86516-352-9.
  • Mason, Herbert (1970). Gilgamesh: A Verse Narrative. Boston: Mariner Books. ISBN 978-0-618-27564-9.
  • Mitchell, Stephen (2004). Gilgamesh: A New English Version. New York: Free Press. ISBN 0-7432-6164-X.
  • Sandars, N. K. (2006). The Epic of Gilgamesh (Penguin Epics). ISBN 0-14-102628-6 - re-print of the Penguin Classic translation (in prose) by N. K. Sandars 1960 (ISBN 0-14-044100-X) without the introduction.
  • Parpola, Simo, with Mikko Luuko, and Kalle Fabritius (1997). The Standard Babylonian, Epic of Gilgamesh. The Neo-Assyrian Text Corpus Project. ISBN 951-45-7760-4 (Volume 1) in the original Akkadian cuneiform and transliteration; commentary and glossary are in English. {{cite book}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  • Ferry, David (1993). Gilgamesh: A New Rendering in English Verse. New York: Farrar, Straus and Giroux. ISBN 0374523835.
  • Damrosch, David (2007) The Buried Book: The Loss and Rediscovery of the Great Epic of Gilgamesh. Henry Holt and Co, ISBN 0-8050-8029-5
  • Jacobsen, Thorkild (1976) The Treasures of Darkness, A History of Mesopotamian Religion, New Haven: Yale University Press, ISBN 0-300-01844-4
  • West, Martin (1997) The East Face of Helicon: West Asiatic Elements in Greek Poetry and Myth, New York: Clarendon Press, ISBN 0-19-815042-3

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Vibao
Gharika