Nenda kwa yaliyomo

Usagara (Misungwi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa maana tofauti ya jina hili angalia hapa Usagara

Usagara ni kata na tarafa ya Wilaya ya Misungwi katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Msimbo wa posta ni 33517.

Usagara ni eneo lenye mwonekano mzuri pamoja na mazingira yanayofurahisha macho lakini, licha ya hayo, binadamu anataka kufanya mabadiliko yake kwa kuchafua mazingira.

Pia ni sehemu rahisi kufikika kwa njia ya barabara kwa sababu ni njia panda ya barabara kuu nne, moja inayoelekea Dar es Salaam, nyingine inayoelekea Geita, inayoelekea Musoma (Mkoa wa Mara) na inayoelekea Mwanza Mjini. Ni umbali wa Km 14 kufikia Mwanza mjini (Sahara).

Kihistoria Usagara Misungwi ni sehemu iliyokaliwa na watemi viongozi wa kabila la Wasukuma. Mtemi maarufu wa mwisho kabla ya kuondolewa kwa utawala wa kitemi alijulikana kama Charles Kafipa Minzemalulu. Aliishi makao makuu yake yaliyo kaskazini mwa kijiji cha usagara umbali wa Km 2 kutoka roundabout palipoitwa Idetemya. Upande wa kusini mwa Usagara kuna kijiji cha Sanjo, mahala ambapo mikutano yote ya kiserikali kipindi cha ukoloni ilifanyika.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 44,220 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,037 waishio humo.[2]

Tangu mwaka 2016 kumekuwa na ongezeko la wakazi: hii inatokana na ongezeko la shughuli za kiserikali, ongezeko la huduma za kijamii zikiwemo shule, zahanati na hivyo kupelekea mwingiliano wa jamii kutoka sehemu mbalimbali. Mwingiliano huo umepelekea kukua kwa shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Isaya Daniel Nkondo, mchumi wa chuo kikuu, mzawa wa Usagara na mfanyabiashara maarufu eneo hilo anasema, "Kufikia mwaka 2025 Usagara itakua moja ya miji mikubwa kanda ya ziwa na yenye kuchangia pakubwa kwenye pato la mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla". Changamoto pekee ni ukosefu wa maji safi na salama. Licha ya uwepo wa ziwa Victoria, Usagara imekuwa na shida kubwa ya maji hivyo kufanya adha kubwa kipindi cha kiangazi.

Wakazi wengi wa Usagara ni wakulima na wafugaji, kama ilivyokuwa kwa tamaduni za wakazi wa Mwanza.

Kata za Wilaya ya Misungwi - Mkoa wa Mwanza - Tanzania

Buhingo | Buhunda | Bulemeji | Busongo | Fella | Gulumungu | Idetemya | Igokelo | Ilujamate | Isenengeja | Kanyelele | Kasololo | Kijima | Koromije | Lubili | Mabuki | Mamaye | Mbarika | Misasi | Misungwi | Mondo | Mwaniko | Nhundulu | Shilalo | Sumbugu | Ukiriguru | Usagara


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Usagara (Misungwi) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.