Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020
| |||||||||||||||||||
| |||||||||||||||||||
|
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020 ulifanyika tarehe 28 Oktoba. Wapiga kura walimchagua Rais, wabunge na Madiwani.[1]
Matokeo ya Uchaguzi wa Rais
[hariri | hariri chanzo]Kufuatana na tangazo la Tume la Uchaguzi la 30 Oktoba matokeo yalikuwa kama yafuatayo[2]:
Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 29,754,699. Waliopiga kura walikuwa 15,091,950 (% 50.72), wasiopiga kura walikuwa 14,662,749 (% 49.28).
Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 15,091,950. Kura 261,755 ziliharibika. Jumla ya kura halali ilikuwa 14,830,195.
- Magufuli alipata kura 12,516,252 (sawa na % 84.40 za kura halali)
- Lissu alipata kura 1,933,271 (sawa na % 13.04 za kura halali)
- Wagombea wengine kwa jumla walipata kura 380,672 (sawa na % 2.57 za kura halali)
Wagombea Urais
[hariri | hariri chanzo]Mgombea | Mgombea Mwenza | Chama | |
---|---|---|---|
Bernard Kamillius Membe | Omar Fakih Hamad [3] | Alliance for Change and Transparency (ACT) | |
Tundu Lissu | Salum Mwalimu Juma | Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) | |
Twalib Ibrahim Kadege | Ramadhan Ali Abdallah | United People's Democratic Party (UPDP) | |
Hashim Rungwe Spunda | Mohammed Massoud Rashid | Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) | |
Leopord Lucas Mahona | Khamis Ali Hassan | National Reconstruction Alliance (NRA) | |
John Magufuli | Samia Suluhu | Chama Cha Mapinduzi | |
Queen Cuthbert Sendiga | Khamis Juma Shoka | Alliance for Democratic Change (ADC) | |
Muttamwega Bhatt Mgaywa | Satia Mussa Bebwa | Sauti ya Umma (SAU) | |
Cecilia Augustino Mwanga | Tabu Mussa Juma | Demokrasia Makini | |
Yeremia Kulwa Maganja | Khamis Haji Ambar | National Convention for Construction and Reform Mageuzi (NCCR Mageuzi) | |
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba | Hamida Huweishil Abdalla | Civic United Front (CUF) | |
Philipo John Fumbo | Zaina Juma Khamis | The Democratic Party (DP) | |
Seif Maalim Seif | Rashid Ligania Rai | Alliance for Tanzania Farmers Party (AFP) | |
Khalfan Mohammed Mazrui | Mashavu Alawi Haji | The Union for Multiparty Democracy (UMD) |
Yaliyofuata
[hariri | hariri chanzo]Baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kumaliza kutangaza matokeo, vyama vikuu vya upinzani viliungana kukataa matokeo hayo na kudai uchaguzi huru na wa haki chini ya tume huru vikataja kasoro nyingi za mchakato mzima wa uchaguzi[4] [5] [6]
Upande wake Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) ulizuia mitandao ya kijamii mbalimbali ili kupunguza mawasiliano hasa kutokana na mauaji yaliyotokea Zanzibar.[5]
Nchi na taasisi mbalimbali zimeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu uchaguzi na matokeo yake [7], [8], [9][10].
Tarehe 10 Novemba 2020, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Haki za Binadamu alitoa tamko kuhusu hali tete ya nchi[11] ambalo lilijibiwa mapema na serikali ya Tanzania[12].
Uchaguzi wa 2020 huhesabiwa kuwa ndiyo mbaya kupita yote. Uligubikwa na hila na mbinu chafu. Mbowe alitoa rai yake juu ya uchaguzi huo kwa kusema, ''Kilochofanyika si uchaguzi ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) .''[13]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vaticannews.va/sw/world/news/2020-07/tume-taifa-uchaguzi-nec-uchaguzi-mkuu-tarehe-28-oktoba-2020.html
- ↑ Tanzania Election 2020: Magufuli wins Tanzania’s presidency for a second term, Citizen 30 Oktoba 2020
- ↑ https://www.nec.go.tz/pages/general-elections
- ↑ Odula, Tom (24 Oktoba 2020). "Observers say Tanzania's presidential vote is already flawed". Associated Press. Iliwekwa mnamo 24 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 "Tanzania opposition loses key seats in vote marred by fraud claim". Al Jazeera (kwa Kiingereza). 2020-10-29. Iliwekwa mnamo 2020-10-30.
{{cite web}}
: CS1 maint: url-status (link) - ↑ Odula, Tom (24 Oktoba 2020). "Observers say Tanzania's presidential vote is already flawed". Associated Press. Iliwekwa mnamo 24 Oktoba 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.thecitizen.co.tz/news/Tanzania-electoral-watch-panel-condemns-arrest-of-opposition-/1840340-5638084-5khvflz/index.html
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/news/US-State-Department-calls-for-investigation-into-poll/1840340-5638052-12tmoowz/index.html
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/news/Common-Wealth-ready-to-help--urges-Tanzania-to-investigate-polls/1840340-5638060-6r88cw/index.html
- ↑ https://www.consilium.europa.eu/en/press/press-releases/2020/11/02/tanzania-declaration-by-the-high-representative-on-behalf-of-the-eu-on-the-elections-in-tanzania/
- ↑ https://www.ohchr.org/en/NewsEvents/Pages/DisplayNews.aspx?NewsID=26489&LangID=E
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-11. Iliwekwa mnamo 2020-11-11.
- ↑ "Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Kauli ya vyama vya upinzani". BBC News Swahili. 2020-10-31. Iliwekwa mnamo 2023-05-12.