Trimurti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu za Trimurti
Trimurti
Trimurti
Trimurti

Trimurti ni fundisho katika dini ya Uhindu linaloonyesha miungu mikuu mitatu kama nguvu moja ya kimungu au kwa lugha nyingine miungu mikuu kama maumbo tofauti ya nguvu moja ya kimungu.

Jina latokana na maneno ya Kisanskrit "tri" (maana yake "tatu") na "murti" (maana yake umbo, mwili, sanamu ya mungu).

Miungu ya Trimurti[hariri | hariri chanzo]

Miungu mikuu inayotazamiwa kama umoja katika Trimurti ni Shiva, Vishnu na Brahma.

Katika fundisho hili Brahma hutazamiwa kama muumba wa ulimwengu, Vishnu kama mungu wa kuutunza na Shiva kama nguvu itakayoharibu dunia na kuipeleka mwisho wake ili kuandaa uumbaji mpya wa dunia safi.

Trimurti inafundisha ya kwamba miungu hiyo si ya pekee na bila ususiano, bali kila mmoja ni sehemu tu ya Brahman yaani ile nguvu moja kubwa.

Sanamu za Trimurti[hariri | hariri chanzo]

Kuna picha na sanamu za Trimurti zinazolenga kuonyesha umoja huu kwa mfano

  • vichwa 3 juu ya shingo 1
  • nyuso 3 kwenye kichwa 1
  • sanamu yenye mwili 1 mwenye vichwa 3 na mikono 6.

Picha hii inaunganishwa mara nyingi na ishara za miungu hii kama vile birika ya maji na rosari (Brahma), diski na konokono (Vishnu) na pembetatu pamoja na ngoma (Shiva).

Mawazo juu ya Trimurti[hariri | hariri chanzo]

Umoja wa miungu kama Trimurti unatajwa katika vitabu vya kale kama Kūrma Purāṇa lakini si mara nyingi. Trimurti inafundishwa pia katika vitabu vya dini vya shule lakini kwa Wahindu wengi haina umuhimu mkubwa, kwa kuwa wengi wao ni hasa wafuasi wa mungu mkuu mmojawapo, ama Vishnu au Shiva au pia nguvu ya kike kwa majina mbalimbali.

Wafuasi wa Shiva hufundisha "Trimurti" lakini hapo kwao ni nyuso 3 za Shiva mwenyewe anayetazamiwa kama muumba, mtunza na mharibu dunia kwa pamoja ingawa kwa kuchukua maumbo mbalimbali.

Kwa hiyo ni zaidi fundisho linalotaka kuimarisha umoja wa Wahindu wote.

Watazamaji waliona ya kwamba mafundisho ya Trimurti inafanana kiasi na mafundisho ya Utatu katika Ukristo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: