Tiglath-pileseri I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Tiglath-pileresi I jinsi ilivyokatwa kwenye mwamba wa mlima na kuonyesha jina lake

Tiglath-pileseri I alikuwa mfalme wa milki ya Ashuru (Assyria) kuanzia mwaka 1114 KK hadi 1076 KK.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina lake kwa lugha ya kwao iliandikwa "Tukulti-apil-esharra I" lakini "Tiglat-pileseri" ni umbo lililo kawaida kutokana na taarifa ya Biblia kuhusu mfalme mwenye jina hilihili Tiglath-pileseri[1] anayetajwa katika Kitabu cha pili cha Wafalme, mlango 16, 7-10.

Jina la Tukulti-apil-esharra lilimaanisha "namsadiki mwana mrithi wa Esharra"; "E-sharra" ilikuwa jina la hekalu muhimu mjini Ashuru na mwana mrithi ilikuwa namna ya kumtaja mungu aliyejulikana kwa jina la "Ashuru"[2] aliyekuwa asili ya jina la mji na milki.

Utawala wake[hariri | hariri chanzo]

Tiglath-pileseri I alifuata siasa ya kushambulia nchi jirani akafaulu kueneza milki yake hadi ndani ya Anatolia (leo Uturuki), katika Syria na hadi ufuko wa Mediteranea.

Baada ya kutwaa miji ya Biblos na Arvad alisafiri pia baharini.

Ashuru ilikuwa milki yenye nguvu kushinda majirani wote kwa karne zilizofuata.

Alipenda uwindaji, alikuwa pia mfalme aliyeagiza ujenzi wa mahekalu na maboma mengi.

Wakati wa kutengenezwa upya hekalu kuu mjini Ashuru mwaka 1109 KK aliagiza kuandikwa taarifa juu ya utawala wake kwa mwandiko wa kikabari ambayo ni hati ya kihistoria ya pekee iliyotunzwa kwa kirefu kutoka enzi zake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Anahesabiwa kama Tiglath-pileseri III
  2. Raymond Edward Brown, Joseph A. Fitzmyer, Roland Edmund Murphy, The Jerome Biblical commentary, Prentice-Hall, 1968, 211

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]