Tiglath-pileseri I
Tiglath-pileseri I alikuwa mfalme wa milki ya Ashuru (Assyria) kuanzia mwaka 1114 KK hadi 1076 KK.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina lake kwa lugha ya kwao iliandikwa "Tukulti-apil-esharra I" lakini "Tiglat-pileseri" ni umbo lililo kawaida kutokana na taarifa ya Biblia kuhusu mfalme mwenye jina hilihili Tiglath-pileseri[1] anayetajwa katika Kitabu cha pili cha Wafalme, mlango 16, 7-10.
Jina la Tukulti-apil-esharra lilimaanisha "namsadiki mwana mrithi wa Esharra"; "E-sharra" ilikuwa jina la hekalu muhimu mjini Ashuru na mwana mrithi ilikuwa namna ya kumtaja mungu aliyejulikana kwa jina la "Ashuru"[2] aliyekuwa asili ya jina la mji na milki.
Utawala wake
[hariri | hariri chanzo]Tiglath-pileseri I alifuata siasa ya kushambulia nchi jirani akafaulu kueneza milki yake hadi ndani ya Anatolia (leo Uturuki), katika Syria na hadi ufuko wa Mediteranea.
Baada ya kutwaa miji ya Biblos na Arvad alisafiri pia baharini.
Ashuru ilikuwa milki yenye nguvu kushinda majirani wote kwa karne zilizofuata.
Alipenda uwindaji, alikuwa pia mfalme aliyeagiza ujenzi wa mahekalu na maboma mengi.
Wakati wa kutengenezwa upya hekalu kuu mjini Ashuru mwaka 1109 KK aliagiza kuandikwa taarifa juu ya utawala wake kwa mwandiko wa kikabari ambayo ni hati ya kihistoria ya pekee iliyotunzwa kwa kirefu kutoka enzi zake.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Inscription of Tiglath-Pileser I. Babylonian and Assyrian Literature. Project Gutemberg.
- Assyrian origins: discoveries at Ashur on the Tigris: antiquities in the Vorderasiatisches Museum, Berlin, an exhibition catalog from The Metropolitan Museum of Art Libraries (fully available online as PDF), which contains material on Tiglath-Pileser I