Tambarare ya Uhindi Kaskazini


Tambarare ya Uhindi Kaskazini ni eneo kubwa la bara upande wa kusini wa Milima ya Himalaya linaloshika Uhindi Kaskazini yote na Bangladesh yote pamoja na sehemu za Pakistan na Nepal.
Tambarare hiyo imesababishwa na mito miwili ya Indus na Ganges na ina kilomita za mraba milioni 2.5[1]. Inakaliwa na watu bilioni 1 yaani sehemu ya saba ya watu wote duniani.
Tambarare yote imegawiwa katika mabeseni ya mito miwili: maji upande wa magharibi huelekea mto Indus na upande wa mashariki huelekea mto Ganges.
Tambarare hiyo inapokea maji yake kutoka milima ya Himalaya hasa; mito hiyo imetelemka pamoja na matope yaliyojenga tabaka nene la ardhi yenye rutuba. Hivyo ni eneo linalofaa kwa kilimo hasa cha mpunga na ngano kinacholisha idadi kubwa ya watu.
Katika historia ya binadamu ilikuwa kati ya maeneo ya kwanza ambako milki na utamaduni wa miji vilianzishwa vikiwezesha kuwepo kwa wataalamu walioweka misingi ya sanaa na elimu ya juu.[2]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ (2014) Farmers preferences for climate-smart agriculture: An assessment in the Indo-Gangetic Plain. Intl Food Policy Res Inst, 2.
- ↑ India. CIA – The World Factbook. Jalada kutoka ya awali juu ya 11 June 2008. Iliwekwa mnamo 14 December 2007.
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tambarare ya Uhindi Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |