Nenda kwa yaliyomo

Mbuga baridi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Steppe)
Mbuga baridi nchini Mongolia.

Mbuga baridi (ing. steppe) ni eneo lenye uoto wa manyasi bila miti, katika tabianchi baridi ya latitudo za kati ambako usimbishaji ni mdogo. Tabianchi hii inaweza kuwa na vipindi vya joto, hata joto kali lakini athira kubwa ni vipindi virefu vya jalidi.

Maeneo makubwa ya mbuga baridi yapo Eurasia (kuanzia Hungaria hadi Siberia), Amerika Kaskazini kati ya Mto Mississippi na milima ya Rocky Mountains [1], Amerika Kusini upande wa mashariki wa milima ya Andes [2] na kusini mwa beseni ya Amazonas.

Majirabaridi huwa na halijoto chini ya 0 °C, majirajoto huwa na ukame.

Tabianchi inayounda mbuga baridi kwa kawaida ni nusuyabisi na ya kibara. Kuna tofauti kubwa kati ya baridi na joto, kama sentigredi 40 °C wakati wa majirajoto na −40 °C wakati wa majirabaridi. Tofauti kubwa zinaweza kutokea katika kipindi cha masaa 24. Kwa mfano katika nyanda za juu za Mongolia inawezekana kupima 30 °C wakati wa mchana na chini ya 0 °C wakati wa usiku.

Kukosekana kwa miti kunatokana hasa na uhaba wa maji. Mvua ni chache. Mbuga baridi uko ndani ya bara kwa umbali mkubwa na bahari, kwa hiyo kiasi cha usimbishaji ni kidogo. Ukame wakati wa majirajoto na baridi wakati wa majirabaridi zinafupisha vipindi vya kukua kwa mimea.

Kama maji yanapatikana karibu na mito au maziwa ya kudumu miti inaweza kutokea. Maana udongo mara nyingi si mbaya. Hasa maeneo ya chernosyom (udongo mweusi) ya Ukraina na Urusi yana umaarufu wa kuwa na rutuba sana yakimwagiliwa.

  1. hapa huitwa "prairie"
  2. hapa huitwa "pampa"

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • Ecology and Conservation of Steppe-land Birds by Manuel B.Morales, Santi Mañosa, Jordi Camprodón, Gerard Bota. International Symposium on Ecology and Conservation of steppe-land birds. Lleida, Spain. December 2004.ISBN 84-87334-99-7
  • "The Steppes". barramedasoft.com.ar. 1998–2008. Iliwekwa mnamo 2008-04-04.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.