Majadiliano:Mbuga baridi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yafuatayo yamenakiliwa kutoka Majadiliano ya mtumiaji:ChriKo

Steppe?[hariri chanzo]

Salaam, natumaini ulikuwa na Pasaka njema! Siku hizi naangalia Urusi kwa sababu ya mgeni wetu.. Nahitaji neno kwa "steppe". Una ushauri? Mbuga wa manyasi? Pori ya manyasi? Pori manyasi? Porinyasi ? Kipala (majadiliano) 22:55, 7 Aprili 2016 (UTC)[jibu]

Salaam. Pasaka yetu haikuwa njema kama tulivyopenda kwa sababu mke wangu hajaweza kutembea bado. "Steppe" ni eneo la manyasi bila miti au lenye miti michache na kwa Kiswahili eneo kama hili linaitwa mbuga. Kama eneo likiwa na miti mingi zaidi linaitwa savana. Pori ni istilahi ya jumla au eneo lenye miti na vichaka. Kwa hivyo nadhani kwamba tafsiri nzuri ya "steppe" ni mbuga. ChriKo (majadiliano) 20:14, 8 Aprili 2016 (UTC)[jibu]
Asante kwa ushauri. Nimesita kutumia "mbuga" maana ni aina ya nchi inayopatikana Afrika. KWANZA Steppe ni aina ya nchi inayopatikana nje tabianchi ya tropiki. Vipi mbuga baridi? PILI nadhani mbuga ni steppe pamoja na aina za savannah, sivyo? Kipala (majadiliano) 19:14, 11 Aprili 2016 (UTC)[jibu]
Kipala, samahani kwa sababu sinakubaliani na wewe. Kwa maoni yangu ukweli kwamba "steppe" haipatikani hapa Afrika siyo sababu ya kutotumia neno "mbuga". "Steppes" ni aina za "grasslands" na katika sehemu nyingine za dunia zinaitwa "prairy", "cerrado" na "grass savanna". Na "grassland" ni mbuga kwa Kiswahili. Kama "pori" likitumika kumaanisha aina maalumu ya mandhari hili ni eneo lenye vichaka vifupi vyingi (kama "maquis" au "karoo"). Kwa hivyo nadhani kwamba kutumia istilahi mpya "pori ya manyasi" si wazo zuri. Ukitaka tumia "mbuga baridi". ChriKo (majadiliano) 22:04, 15 Aprili 2016 (UTC)[jibu]
Asante, twende mbuga baridi. Kipala (majadiliano) 14:07, 16 Aprili 2016 (UTC)[jibu]