Skype

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Skype
Nembo ya Skype

Skype (matamshi: / skaɪp /) ni programu ambayo inatumia intaneti kupiga simu za sauti na video kwa teknolojia inayoitwa Voice over Internet Protocol (VoIP). Skype huwezesha watumiaji kutuma ujumbe wa maneno, video, sauti, picha na kufanya mikutano kwa video.

Iliundwa mwaka 2003 na Mswidi na Mdenmark Niklas Zennström na Janus Friis wakishirikiana na Waestonia Ahti Heinla, Priit Kasesalu, na Jaan Tallinn, na kwa sasa inaendeshwa na kampuni ya huko Luxemburg inayoitwa Skype Technologies SARL, ambayo tangu mwaka k2011 ni sehemu ya Microsoft.

Kabla ya kumilikiwa na Microsoft, Skype ilimilikiwa na eBay kuanzia Septemba 2005 hadi 2011. eBay iliinunua kutoka kwa walioizindua kwa dola za Kimarekani bilioni 2.6 miaka 2 baada ya kuzinduliwa.[1] [2]

Mwaka wa 2009, eBay iliuzia Silver Lake, Andreessen Horowitz, na Bodi la Mipango ya Uwekezaji wa Pensheni la Kanada asilimia 65 ya hisa za Skype kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 1.9 wakati thamani ya Skype ilikuwa takriban dola za Kimarekani 2.75.

Tarehe 10 Mei 2011, Microsoft ilianza mipango ya kumiliki Skype Communications, S.à r.l kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 8.5 na tarehe 13 Oktoba mwaka huo mipango ya umiliki ikakamilika.[3][4]

Jina Skype linatokana na "Sky peer-to-peer" ambapo ilifupishwa kuwa "Skyper". Hata hivyo, anuani ya tovuti yenye jina hilo ilikuwa tayari imenunuliwa na kampuni nyingine,[5] hivyo herufu "r" iliondolewa na kuwa Skype.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. EBay to buy Skype in $2.6bn deal. BBC (12 September 2005). Iliwekwa mnamo 2 October 2014.
  2. Canada Pension plan buys Skype stake | Toronto Star. Thestar.com (2 September 2014). Iliwekwa mnamo 21 August 2014.
  3. Microsoft to Acquire Skype - About Skype. web.archive.org (2011-05-12). Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-05-12. Iliwekwa mnamo 2019-06-14.
  4. Toor Amar (2011-11-13). Microsoft finalizes acquisition of Skype, Tony Bates shares his thoughts (video) (en). Engadget. Iliwekwa mnamo 2019-06-14.
  5. The World's Hottest VC?. Jalada kutoka ya awali juu ya 9 January 2008.
  6. Origin of the name/word Skype. Jalada kutoka ya awali juu ya 4 November 2005. Iliwekwa mnamo 13 August 2010.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Skype kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.