Niklas Zennström

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Niklas Zennström

Niklas Zennström (alizaliwa 16 Februari 1966) ni bilionea mjasiriamali wa Uswidi anayejulikana zaidi kwa kuanzisha kampuni mbalimbali za intaneti akishirikiana na Janus Friis zikiwemo Skype na Kazaa. Hivi karibuni alianzisha kampuni ya uwekezaji ya Atomico.

Zennström pia ni mmoja wa waanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Zennström Philanthropies.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Zennström ana shahada toka Chuo Kikuu cha Uppsala na KTH Royal Institute of Technology.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Zennström alianza kazi mwaka 1991 kwenye shirika la simu la Tele2. Aliwahi pia kuwa mkurugenzi wa kampuni ya everyday.com.

Mwaka 2000 Zennström na Janus Friis walianzisha Kazaa. Baada ya wanamuziki na watoa filamu nchini Marekani kufungua kesi dhidi ya Kazaa, kampuni hii ilinunuliwa na Sharman Networks.

Baadaye Zennström alianzisha kampuni ya Joltid na Altnet.

Mafanikio makubwa ya Zennström hadi leo ni kampuni ya Skype. Oktoba 2005 Skype ilinunuliwa na eBay kwa pauni bilioni 2.1. Zennström alikuwa mkurugenzi wa Skype hadi Septemba 2007. Baada ya kuuza Skype, Zennström alianzisha kampuni ya Joost, huduma ya kusambaza video kwenye intaneti, mwaka 2007.

Mwaka 2009 Zennström alikuwa mmoja wa wawekezaji walionunua Skype Technologies toka kwa eBay. Hivi sasa, Zennström anaongoza kampuni ya Atomico. Kampuni hii, yenye makao yake makuu nchini Uingereza inawekeza kwenye kampuni za teknolojia zinazokua kwa kasi. KupitiaAtomico wamewekeza kwenye zaidi ya kampuni 50 kwenye mabara manne zikiwemo kampuni za Supercell, Rovio, Last.fm, Fon, Rdio, Fab, Klarna na Skype.

Mei 2011 Skype ilinunuliwa na Microsoft kwa dola bilioni 8.5. Inaaminika kuwa Zennström na Friis walijipatia dola bilioni 1.[1]

Novemba 2014 Zennström aliingizwa kwenye SUP46's Swedish Startup Hall of Fame.[2]

Mahojiano[hariri | hariri chanzo]

 • Business Week (19 September 2005) [3]
 • The Guardian (14 July 2005) [4]
 • PCTechTalk (10 July 2005) [5]
 • BusinessWeek Online (30 May 2005) [6]
 • IDG News Service (16 March 2005) [7]
 • PC Pro (11 March 2005) [8]
 • TMCnet (2 March 2005) [9]
 • Engadget (8 November 2004) [10]
 • Pocket PC Thoughts (3 September 2004) [11]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Malik, Om (2011-05-09). Why Microsoft Is Buying Skype for $8.5 Billion (en-US).
 2. Niklas Zennström inducted into SUP46's Swedish Startup Hall of Fame as the startup hub celebrated its first year - Swedish Startup Space. Jalada kutoka ya awali juu ya 4 March 2016.
 3. Archived copy. Jalada kutoka ya awali juu ya 11 March 2007. Iliwekwa mnamo 2006-10-21.
 4. Interview by Hamish Mackintosh (2005-07-14). Talk time: Niklas Zennström | Technology | The Guardian. Technology.guardian.co.uk. Iliwekwa mnamo 2017-05-08.
 5. Archived copy. Jalada kutoka ya awali juu ya 23 October 2006. Iliwekwa mnamo 2006-10-21.
 6. Archived copy. Jalada kutoka ya awali juu ya 27 August 2006. Iliwekwa mnamo 2006-10-21.
 7. Archived copy. Jalada kutoka ya awali juu ya 11 March 2007. Iliwekwa mnamo 2006-10-21.
 8. Archived copy. Jalada kutoka ya awali juu ya 16 October 2007. Iliwekwa mnamo 2006-11-06.
 9. Rich Tehrani (2005-03-02). Skype Interview. Voip-blog.tmcnet.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-06-24. Iliwekwa mnamo 2017-05-08.
 10. The Engadget Interview: Niklas Zennström. Engadget.com (2004-11-08). Iliwekwa mnamo 2017-05-08.
 11. Windows Phone Thoughts: Talking Free, Wirelessly: Interview with Niklas Zennström, CEO of Skype Ltd. Pocketpcthoughts.com (2004-09-03). Iliwekwa mnamo 2017-05-08.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Niklas Zennström kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.