Nenda kwa yaliyomo

Siprila wa Kurene

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Siprila wa Kurene (alifariki Kurene, leo nchini Libya, 300 hivi) ni kati ya Wakristo waliouawa kikatili wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian.

Alipokataa kutoa sadaka kwa miungu, walimtia mkononi ubani na makaa ya moto ili kwa kuvidondosha altareni kutokana na maumivu aonekane kama kwamba amekubali; kumbe yeye aliyashikikilia muda mrefu. Baada ya hapo aliteswa kwa ukatili hadi kufa[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Julai[2][3].

Inaonekana ni yule mjane Sirila wa Kurene anayeheshimiwa kama mtakatifu mfiadini tarehe hiyohiyo[4]. Pengine wanatajwa pamoja naye Aroa na Lusia[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.