Nenda kwa yaliyomo

Mzee Simeoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Simeoni Mwenye Haki)
Simeone Mpokea Mungu kadiri ya Alexei Egorov, 1830 n.k.

Mzee Simeoni alikuwa mwanamume mwadilifu wa Yerusalemu (leo nchini Palestina/Israeli) katika karne ya 1 KK.

Ni maarufu hasa kwa kumpakata mtoto Yesu alipoletwa na wazee wake katika hekalu la Yerusalemu siku 40 tu baada ya kuzaliwa Bethlehemu.

Kadiri ya Injili ya Luka (2:25-35[1]) alikwenda kumlaki kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu aliyekuwa amemuahidia hatakufa kabla hajamuona Masiya.

Alipomtambua katika mtoto huyo alishangilia na kumsifu Mungu kwa wimbo maarufu alipomtangaza Yesu kuwa ndiye wokovu ulioandaliwa kwa mataifa yote.

Baada ya hapo alimtabiria Bikira Maria kwamba upanga utamchoma moyo kuhusiana na upinzani utakaompata mwanae.

Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu, hasa tarehe 2, 3[2] au 15 Februari.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 2:22 Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Mose, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana. 23 Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: "Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana." 24 Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana. 25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. 26 Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Masiha wa Bwana. 27 Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia Hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na Sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu na kusema: 29 "Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani. 30 Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu utokao kwako, 31 ambao umeutayarisha mbele ya watu wote: 32 Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli." 33 Baba na mama yake Yesu walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto. 34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, "Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; 35 na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako."
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzee Simeoni kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.