Simeoni Mwanateolojia Mpya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Simeoni Mwanateolojia Mpya

Simeoni Mwanateolojia Mpya (kwa Kigiriki: Συμεὼν ὁ Νέος Θεολόγος; Basileion, Galatia, 949Paloukiton, 12 Machi 1022) alikuwa mmonaki na mshairi wa Byzanti.

Alipewa sifa "Mwanateolojia" si kutokana na elimu yake, bali kwa sababu ya kufundisha kwa dhati juu ya Mungu kutokana na mang'amuzi yake katika sala, kama walivyofanya Mtume Yohane na Gregori wa Nazianzo. Mojawapo ya mafundisho aliyosisitiza ni kwamba wote wanatarajiwa kufikia mang'amuzi hayo.

Maandishi yake ni kama vile Tenzi za Upendo wa Mungu, Hotuba za Kimaadili na Hotuba za kikatekesi.

Sehemu nzuri zaidi ziliingizwa katika Filokalia na kwa njia hiyo zimeathiri zaidi maisha ya kiroho ya Wakristo wengi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Tafsiri za Kiingereza za maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.