Sila

Mtakatifu Sila au Siluano (kwa Kigiriki: Σίλας / Σιλουανός; karne ya 1 AD) ni mmojawapo kati ya viongozi muhimu zaidi wa Kanisa la mwanzo huko Yerusalemu.
Kutoka huko alitumwa mara nyingi kushughulikia matatizo mbalimbali (kuanzia Mdo 15:22) akawa mwenzi wa Mtume Paulo katika safari za kimisionari (kuanzia Mdo 16:25).
Anatajwa katika barua zake mbalimbali (k.mf. 2Kor 1:19).
Hatimaye alimsaidia Mtume Petro kuandika waraka yake wa kwanza (1 Pet 5:12).[1]
Anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu, ila tarehe ya sikukuu ni tofautofauti. Kwa Wakatoliki ni tarehe 13 Julai[2].
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Notes on 1 Peter. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-10-03. Iliwekwa mnamo 2012-08-14.
- ↑ Martyrologium Romanum
![]() |
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sila kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |