Shirikisho la Soka Tanzania
'Shirikisho la Soka Tanzania' (au 'Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania: kwa Kiingereza: Tanzania Football Federation' au [[kifupi]: 'TFF') ni shirikisho la kitaifa linalosimamia masuala ya mpira wa miguu nchini Tanzania, ikihusisha Ligi Kuu Tanzania Bara na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars. Ilianzishwa mwaka 1945 na kusajiliwa kuwa mwanachama wa FIFA mwaka 1964. Raisi wa sasa wa shirikisho ni Wallace Karia.[1].
Shule za Michezo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Januari 2008 shirikisho la soka Tanzania kupitia udhamini wa Peter Johnson walianzisha shule ya michezo nchini Tanzania mahususi kwa ajili ya mpira wa miguu maarufu kwa jina la (TSA), shule hoii inalenga kukuza vipaji vya soka nchini Tanzania na inatoa udhamini wa kimasomo kwa wachezaji wadogo.[2][3][4]
Uwanja wa Taifa
[hariri | hariri chanzo]Uwanja wa taifa wa Tanzania upo jijini Dar es Salaam. Ulifunguliwa mwaka 2007 ukiwa umepakana na uwanja wa Uhuru, ambao ndio uliokua uwanja wa taifa hapo kabla. Michezo mingi ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na michezo ya nyumbani ya timu ya taifa inachezewa katika uwanja huo.
Maraisi
[hariri | hariri chanzo]- Ali Chambuso 1967-1974
- Said El MaaBwny 1974-1987
- Mohamed Mussa 1987-1992
- Muhidn Ndolanga 1992-2004
- Leodgar Tenga 2004-2013
- Jamal E Malinzi 2013-2017
- Wallace Karia 2017–hadi sasa
Ligi Kuu Tanzania Bara
[hariri | hariri chanzo]Ligi Kuu Tanzania Bara ina jumla ya timu 16 zinazoshiriki katika mashindano, Timu hizo ni pamoja na:[5]
- Yanga S.C.
- Simba S.C.
- Kagera Sugar F.C.
- Ihefu F.C.
- Tabora United F.C.
- Mtibwa Sugar F.C.
- Azam F.C.
- Tanzania Prisons F.C.
- Costal Union
- Dodoma F.C.
- Namungo FC
- JKT Tanzania F.C.
- MASHIJAA F.C
- KMC F.C.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ {cite web|last=Muga |first=Emmanuel |url=https://www.bbc.com/sport/0/football/24734997 |title= Jamal Malinzi elected Tanzania FA president |publisher=Bbc.co.uk |date= |accessdate=2014-01-22}}
- ↑ Muga, Emmanuel. "BBC Sport - Tanzanian FA to "focus on football development"". Bbc.co.uk. Iliwekwa mnamo 2013-11-15.
- ↑ Muga, Emmanuel (2013-05-10). "BBC Sport - Tanzania Football Federation sets new election dates". Bbc.co.uk. Iliwekwa mnamo 2013-11-15.
- ↑ "Nyamlani highlights 9 priorities | 24 Tanzania News". 24tanzania.com. Iliwekwa mnamo 2013-11-15.
- ↑ ["African Soccer Union African Soccer Union, Tanzania (Kiingereza)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-20. Iliwekwa mnamo 2009-08-04. African Soccer Union African Soccer Union, Tanzania (Kiingereza)]
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti katika African Soccer Union Ilihifadhiwa 20 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine.
- Tanzania katika FIFA.com Ilihifadhiwa 7 Aprili 2014 kwenye Wayback Machine.
- Tanzania Sports
- Tanzania katika CAF Online
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Shirikisho la Soka Tanzania kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |