Nenda kwa yaliyomo

Ihefu F.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ihefu F.C. ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Tanzania iliyopo mkoani Mbeya. Makao makuu ya klabu hiyo ni Wilaya ya Mbarali kata ya Ubaruku ambapo ndipo ulipo uwanja wa klabu hii.

Kwa sasa michezo yao ya nyumbani inachezwa kwenye Uwanja wa Highlands Estates Stadium, uliopo Ubaruku wilayani Mbarali, mkoa wa Mbeya.

Ihefu imeanzishwa mnamo mwaka 2012. Ilipambana kucheza ligi daraja la pili (SDL) Na ligi daraja la kwanza (FDL) ikafanikiwa kupanda daraja mwaka 2019, Baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi A la FDL na kucheza Play off dhidi ya Mbao F.C.. Ihefu ilishinda mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Mbao katika mguu wa kwanza uliopgwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Ihefu na mguu wa 2 walipigwa mabao manne kwa mawili, hivyo kufanya aggregate iwe 4-4 na kumfanikisha Ihefu kupanda daraja kwa faida ya magoli ya ugenini.

Msimu wa 2020/21 ilishiriki Ligi Kuu Tanzania bara ila ikashuka daraja baada ya kumaliza msimu nafasi ya 17 ikikusanya alama 35 katika michezo 34, ilishinda michezo 9, droo 8 na kupoteza michezo 17 huku ikifunga magoli 22 na kuruhusu magoli 41. Msimu huo zilishuka timu 4: Ihefu Sc, Gwambina Fc, JKT Tanzania Fc na Mwadui Fc.

Tarehe 4 Oktoba 2023 Ihefu iliifunga Yanga mara ya pili kama timu pekee iliyowahi kuharibu utaratibu wa Yanga kutokufungwa na timu yoyote kwenye msimu uliopita. Yanga inaonekana ni timu dhaifu kwa Ihefu.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Ihefu F.C. kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.