Tanzania Prisons F.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tanzania Prisons F.C.
Prisons FC.jpg
Jina kamiliTanzania Prisons F.C.
Jina la utaniWajelajela
UwanjaUwanja wa michezo wa Sokoine
(Uwezo: 20000)
MmilikiJeshi la Magereza Tanzania Bara
LigiLigi Kuu Tanzania Bara

Tanzania Prisons F.C. ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Tanzania iliyopo mkoani Mbeya na inamilikiwa na Jeshi la Magereza Tanzania Bara.

Michezo yao ya nyumbani inachezwa kwenye uwanja wa michezo wa Sokoine.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Prisons miaka ya nyuma ilikuwa ikijulikana kama Chuo Ruanda SC chini ya Kocha Katikilo kabla ya mwaka ya 1995 kuitwa Tanzania Prisons SC ikashiriki Ligi Daraja la Kwanza, chini ya Kocha Hassan Mlilo na baadaye ilifundishwa na kocha wa zamani wa Simba, marehemu Paul West Gwivaa mwaka wa 1997.[1]

Mwaka 1999 ikiwa chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa na msaidizi wake, Freddy Felix ‘Minziro’ ilibeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mwaka 2000 ilishiriki Klabu Bingwa Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa Afrika) na kutolewa hatua ya awali. Pia, ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwaka wa 2005 na 2006 na katika hatua zote haikufanya vizuri ilitolewa hatua ya awali.

Mwaka 2009 ilishuka daraja na kufanikiwa kupanda mwaka 2011 chini ya Kocha Stephen Matata.

Timu inavaa jezi rangi ya kijani yenye mchanganyiko na nyeupe.

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Klabu hiyo iliweza kutwaa kombe la Ligi kuu ya Tanzania: 1 mwaka 1999.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Tanzania Prisons F.C. kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Kuporomoka kwa Tanzania Prisons", Mwanaspoti (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2022-06-20