Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa michezo wa Sokoine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa Sokoine ni uwanja wa michezo uliopo katika kata ya Sisimba, mkoa wa Mbeya nchini Tanzania unaomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).[1][2]

Uwanja huo ulijengwa mwaka 1984 na unatumika kwa mambao mawili, mpira wa miguu na hafla za kitaifa au mikutano. Kwa mara ya kwanza uwanja huu ulikuwa ukijulikana kama Mapinduzi Stadium, lakini mwaka 1984 ulibadilishwa jina baada ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Edward Sokoine.

Uwanja huu unatumika kama uwanja wa nyumbani wa timu mbili ambazo ni Prisons F.C. na Mbeya City F.C. ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000.

  1. Muga, Emmanuel (17 Agosti 2014). "CCM should facelift its venues before VPL starts". Na. The Citizen. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-28. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2017.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-28. Iliwekwa mnamo 2023-05-14.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Sokoine kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.