Nenda kwa yaliyomo

Mbeya City F.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mbeya City Football Club ni klabu ya soka ya mjini Mbeya, Tanzania, inayocheza katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Timu hiyo ilianzishwa mwaka 2011 katika Jiji la Mbeya ambalo liko katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa Tanzania.

Mbeya city ilianza kushiriki Ligi kuu ya Vodacom mnamo mwaka 2013 ndio ulikuwa msimu wake wa kwanza pia ilicheza soka la kuvutia kwa kushika nafasi ya tatu pia Mbeya City ina wachezaji vijana wanaochipukia kwa sasa Mbeya City ni timu yenye ubora kwa kucheza soka la kuvutia.

Mbeya City FC inajulikana kwa majina mengi kama vile Green City Boys, Tigers Purple na Jacaranda Worriors.

Jezi yao ya nyumbani ni rangi ya zambarau na nyeupe.

Uwanja wa klabu hiyo unaitwa Sokoine ambao unaweza kuweka watu 20,000.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Mbeya City F.C. kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.