Seneti ya Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Seneti ni chumba cha juu cha Bunge la Kenya. Seneti ilianzishwa mara ya kwanza katika katiba ya Kenya ya mwaka 1963. Baada ya kupigwa marufuku mwaka 1966, Seneti ilirudishwa katika katiba mpya ya Kenya, mwaka 2010.

Seneti ya Kwanza, 1963-1966[hariri | hariri chanzo]

Katiba ya Kenya ya 1963 ilitengeneza Seneti iliyokuwa na maseneta 41 waliochaguliwa kwa muda wa miaka sita, na theluthi moja ya wajumbe wa kustaafu kila baada ya miaka miwili. Timotheo Chokwe alikuwa spika wa kwanza wa Seneti hiyo.[1] Seneti ilifanywa marufuku mwaka wa 1966, wakati wa uanachama wake uliunganishwa pamoja na ule wa Jumba la wawakilishi kuunda Bunge lenye chumba kimoja.

Seneti ya Kisasa, 2013–sasa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 2013, uchaguzi wa Seneti ulifanyika tarehe 4 Machi 2013.[2] Chini ya katiba mpya, ambayo ilipitishwa wakati wa kura ya maoni ya mwaka 2010, uchaguzi mkuu wa 2013 ndio ulikuwa wa kwanza kujumuisha Maseneta wanaowakilisha kaunti 47. Ulikuwa pia uchaguzi mkuu wa kwanza wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Kulingana na sehemu yao ya nafasi za kuchaguliwa, vyama vya siasa viliteua wanawake 16. Uteuzi wa ziada ulifanyiwa wajumbe wawili kuwawakilisha vijana na wawakilishi wawili kuwakilisha watu wenye ulemavuSpika, ambaye si seneta, huchaguliwa na Maseneta na kuapishwa katika siku ya kwanza ya kikao cha Seneti.

Nguvu[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Europa World Year Book 1965, p. 638
  2. "Kenya to hold polls in March 2013, says elections body", The Citizen, 18 March 2012. Retrieved on 2 September 2012. Archived from the original on 2012-07-05. 

Anwani ya kijiografia: 1°17′20″S 36°49′22″E / 1.2888°S 36.8227°E / -1.2888; 36.8227