Nenda kwa yaliyomo

Sefania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Kirusi ya karne ya 18.
Sefania akihubiri (mchoro toka Ufaransa, karne ya 16.

Nabii Sefania (kwa Kiebrania צְפַנְיָה yaani "Aliyefichwa na Mungu") alikuwa mwana wa Kushi, mtu wa Yerusalemu aliyehubiri kwa nguvu miaka 640-625 hivi KK, yaani mwanzoni mwa utawala wa mfalme Yosia, kabla huyo hajaanza urekebisho wake wa kidini uliofuata kuvumbua hekaluni maandiko ya Kumbukumbu la Sheria.

Ni wakati uleule aliofanya kazi nabii Yeremia, ambaye analingana naye sana.

Habari zake zinatokana tu na kitabu chake ambacho ni cha tisa kati ya vile 12 vya Manabii Wadogo.

Pamoja na kutisha kwa matabiri yake dhidi ya maovu ya watu wa Yuda, yatakayoadhibiwa katika siku ya hasira ya Bwana, alifariji watu maskini na walionewa kwa kuwapa tumaini la wokovu kwamba wao ndio watakaobaki katika Israeli (3:9-20)[1].

Ndio mwanzo wa imani ya kuwa wapenzi wa Mungu ni hasa fukara, ambayo taratibu ilitia mizizi katika Israeli hadi ilipokuja kukaziwa na Yesu (Lk 6:20-21).

Tangu kale Sefania anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Desemba[2][3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sefania kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.