Saint-Denis (Reunion)
Saint-Denis | |||
| |||
Majiranukta: 20°52′44″S 55°26′53″E / 20.87889°S 55.44806°E | |||
Nchi | Réunion | ||
---|---|---|---|
Idadi ya wakazi | |||
- Wakazi kwa ujumla | 197,464 | ||
Tovuti: www.saintdenis.re |
Saint-Denis (au Saint-Denis de la Réunion) ni mji mkuu wa eneo la ng’ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa: "département d'outre-mer") la Réunion ambayo ni kisiwa kimojawapo cha funguvisiwa la Maskarena katika Bahari Hindi.
Saint-Denis ni pia mji mkubwa wa kisiwa ukiwa na wakazi 131,557 (mwaka 1999).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Saint-Denis ilianzishwa na Mfaransa Étienne Régnault mnamo mwaka 1669 ikawa mji mkuu wa kisiwa mwaka 1738.
Saont-Denis ni makao makuu ya jimbo la Kanisa Katoliki ambalo zamani lilienea kutoka pwani za Somalia hadi Madagaska pamoja na visiwa vyote vya Bahari Hindi. Kwa msingi huo askofu wake alituma kisiwani Zanzibar (leo nchini Tanzania) wamisionari wa kwanza wa karne ya 19 ambao wamekuwa chanzo cha Kanisa hilo Afrika Mashariki.
Mwaka 1860 Zanzibar ilitengwa pamoja na pwani ya Afrika ya Mashariki kuwa jimbo dogo la pekee, sawa na ilivyokuwa kwa Madagaska tangu mwaka 1841.[1]
Usafiri
[hariri | hariri chanzo]Kuna kiwanja cha ndege cha Aéroport de la Réunion Roland Garros ambayo ni geti la kisiwa kwa safari za kimataifa.
Bandari kuu ya kisiwa iko Pointe-des-Galets nje ya mji.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Saint-Denis, mji wa Ufaransa karibu na Paris
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Diocese of Saint-Denis-de-La Réunion, Dioecesis S. Dionysii Reunionis, tovuti ya .catholic-hierarchy.org, iliangaliwa Februari 2018
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ukurasa rasmi wa mji (Kifaransa)