Nenda kwa yaliyomo

Maskarena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Visiwa vya Makarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

Maskarena ni funguvisiwa katika Bahari Hindi takriban km 900 mashariki kwa Madagaska. Kwa jumla ni visiwa vya dola la Morisi pamoja na kisiwa cha Kifaransa cha Réunion.

Visiwa muhimu ni Morisi, Réunion, Rodrigues na Cargados Carajos.

Asili ya jina ni nahodha Mreno Pedro Mascarenhas aliyekuwa Mzungu wa kwanza wa kuvitembelea. Havikuwa na wakazi lakini Mascarenhas alitoa taarifa ya kwamba alikuta mabaki ya meli iliyowahi kuharibika kitambo.

Kwa hiyo inaaminika ya kwamba mabaharia Waarabu labda pia Wahindi waliwahi kufika mara kwa mara visiwani bila kuanzisha makao ya kudumu. Lakini visiwa vilisaidia waliosafiri baharini kupata chakula na maji na kupumzika kabla ya kuendelea na safari zao.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maskarena kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.