Ruaruke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ruaruke ni kata ya Wilaya ya Kibiti katika Mkoa wa Pwani, Tanzania yenye postikodi namba 61812[1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,229 [2] walioishi humo.

Wakazi ni hasa Wandengereko na Wamyagatwa (Wazaramo) pia kuna makabila mengine ya wahamiaji kama vile Wasukuma, Wamang'ati na Waha.

Dini kuu ni Uislamu na Ukristo.

Wakazi wa Ruaruke wanajishughulisha zaidi na kilimo pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mazao yanayolimwa ni ya biashara na chakula. Mazao ya biashara ni korosho, ufuta na mihogo. Mazao ya chakula ni mpunga na mahindi; mihogo hutumika kama zao la chakula na biashara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kibiti - Mkoa wa Pwani - Tanzania
Flag of Tanzania.svg

Bungu | Dimani | Kibiti | Kiongoroni | Mahege | Maparoni | Mbuchi | Mchukwi | Mjawa | Mlanzi | Msala | Mtawanya | Mtunda | Mwambao | Ruaruke | Salale


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ruaruke kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.