Rosh Hashanah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ishara za sikukuu ya Rosh Hashanah: Shofar, komamanga, divai, tofaha na asali

Rosh Hashanah (kwa Kiebrania: רֹאשׁ הַשָּׁנָה, Rōʾš hašŠānā, yaani "mwanzo wa mwaka") ni siku ya kwanza ya mwaka wa Kiyahudi. Ni sikukuu ya kwanza katika mfuatano wa siku takatifu za Uyahudi kwenye mwanzo wa mwaka jinsi zilivyobainishwa na Mambo ya Walawi 23:23–25 [1]. Tarehe yake hutokea kwa kawaida katika mwezi wa Septemba, hadi 5 Oktoba.

Rosh Hashanah ni maadhimisho na sherehe ya siku mbili ambayo huanza siku ya kwanza ya mwezi wa Tishri, ambao ni mwezi wa saba baada ya Pasaka ya Kiyahudi. Hukumbuka uumbaji wa Adamu na Hawa waliokuwa watu wa kwanza kufuatana na taarifa ya Biblia.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Rosh ni neno la Kiebrania kwa "kichwa", ha ni kibainishi (kama "the" ya Kiingereza), na shana inamaanisha "mwaka". Hivyo Rosh HaShanah inamaanisha "mwanzo wa mwaka" na hivyo ni sikukuu ya Kiyahudi ya Mwaka Mpya.[2][3]

Rosh Hashanah inaashiria mwanzo wa mwaka mpya katika kalenda ya Kiebrania ambapo mwaka unapokea jina jipya. Huu ni mwaka wa kiraia, tofauti na miaka mingine inayopatikana ndani ya kalenda ya Kiyahudi. Mwaka wa kiraia ni tofauti na mwaka wa kidini unaoamulia tarehe za sikukuu. Hii ni pia sababu kwamba mwezi Tishri ambamo Rosh Hashana ni tarehe ya kwanza huitwa "mwezi wa saba". [4] Ni mwaka mpya kwa watu, wanyama, na mikataba ya kisheria.

Rosh Hashanah inaadhimisha uumbaji wa watu. [5]

Mzee wa Kiyahudi akipiga tarumbeta ( shofar )
Vyakula vya pekee vya Rosh Hashanah: Tufaha zilizotumbukizwa kwenye asali, makomamanga, divai kwa ajili ya sala ya kiddush.

Desturi za Sikukuu[hariri | hariri chanzo]

Desturi za Rosh Hashanah ni pamoja na kupiga shofar (pembe ya kondoo dume iliyosafishwa), kama ilivyoagizwa katika Torati, kufuatia maagizo ya Biblia ya Kiebrania ya "kupiga baragumu" kwenye Yom Teruah[6] . Desturi zake ni pamoja na kuhudhuria ibada ya sinagogi, pamoja na kufurahia milo ya sikukuu; kwa mfano tufaha zilizowekwa kwenye asali, kutarajia kuamsha mwaka mpya mtamu.

Tarehe[hariri | hariri chanzo]

Tarehe ya Rosh Hashanah inacheza kwa mujibu wa Kalenda ya Gregori kwa sababu miezi ya Kiyahudi inalingana na mwonekano wa Mwezi angani.

Rosh Hashanah hutokea siku 163 baada ya siku ya kwanza ya Pasaka, na hivyo kwa kawaida (lakini si mara zote) huamuliwa na mwezi mpya ulio karibu zaidi na ikwinoksi ya Septemba.

Kwa mujibu wa kalenda ya Gregori, tarehe ya kwanza kabisa ambapo Rosh Hashanah inaweza kutokea ni 5 Septemba, kama ilivyotokea mwaka wa 1842, 1861, 1899, na 2013. Tarehe ya mwisho ambapo Rosh Hashanah inaweza kutokea ni 5 Oktoba, kama ilivyotokea mwaka wa 1815, 1929, na 1967, na itatokea tena mwaka wa 2043.

Baada ya mwaka 2089, tofauti kati ya kalenda ya Kiyahudi na kalenda ya Gregori itasababisha Rosh Hashanah kutokea si mapema zaidi ya 6 Septemba. Kuanzia 2214, tarehe mpya ya mwisho itakuwa 6 Oktoba. [7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Leviticus 23:23–25:HE
  2. "rosh hashanah". Origin and meaning of phrase rosh hashanah by Online Etymology Dictionary. Iliwekwa mnamo 29 September 2019.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. [What Is Rosh Hashanah? – The Jewish New Year, anniversary of the creation of Adam and Eve, a day of judgment and coronation, and sounding of the shofar, "What Is Rosh Hashanah? – The Jewish New Year, anniversary of the creation of Adam and Eve, a day of judgment and coronation, and sounding of the shofar ... – High Holidays"]. Chabad Lubavitch. 27 August 2019. Iliwekwa mnamo 1 September 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "What Is Rosh Hashanah? – The Jewish New Year, anniversary of the creation of Adam and Eve, a day of judgment and coronation, and sounding of the shofar ... – High Holidays". Chabad Lubavitch. 27 August 2019. Iliwekwa mnamo 1 September 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. Chein, Rochel (27 August 2019). "High Holidays". Why is Rosh Hashanah considered the Jewish New Year?. Iliwekwa mnamo 1 September 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu la ukumbusho litakaloadhimishwa kwa kupiga baragumu." (mambo ya Walawi 23,24; tafsiri nyingine za biblia zinasema hapa "tarumpeta" lakini lazima iwe pembe la kondoo dume yaani baragumu )
  7. "An early Rosh HaShanah? – Ask the Rabbi". Oztorah.com. Iliwekwa mnamo 10 September 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]