Baragumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mpigaji baragumu kwenye kisiwa cha Timor
Mpigaji siwa nchini Kongo, mnamo mwaka 1910

Baragumu ni pembe ya mnyama kama vile ng'ombe au kondoo iliyosafishwa na kutobolewa tundu karibu na ncha yake. Inapigwa kwa kupuliza hewa katika tundu na hivyo kutoa sauti. Kiasili baragumu zilitumiwa ili kutumbuiza au kutoa taarifa.

Baragumu mashuhuri ni siwa katika utamaduni wa Waswahili ambayo ni pembe ya ndovu iliyotumiwa kama ishara ya watawala[1].

Baragumu nyingine inayojulikana sana ni shofar ya Wayahudi, ambayo ni pembe ya kondoo dume inayopigwa siku ya Rosh Hashanah[2].

Neno baragumu linatumiwa sasa pia kwa ala za muziki zinazofanana na tarumpeta zikitengenezwa kwa metali.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 5 Reasons Why the Siwa Side-Horn Will Blow Your Mind, tovuti ya artsandculture, iliangaliwa Septemba 2022
  2. Zaburi 81,3 "Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume wakati wa Mwandamo wa Mwezi."