Usubi-nondo
Usubi-nondo | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Usubi-nondo wa bafu (Clogmia albipunctata)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Makabilia 6:
|
Usubi-nondo, visubi-nondo au nzi-nondo (kutoka kwa Kiing. moth flies) ni mbu wadogo wa nusufamilia Psychodinae katika familia Psychodidae ya oda Diptera walio na mabawa makubwa yakilinganishwa na saizi ya mwili na nywele nyingi kama nondo. Spishi fulani, kama Clogmia albipunctata, hujulikana sana, kwa sababu wako kawaida ndani ya mabafu na vyoo za watu ambapo lava wao wanaishi katika mabomba ya kuondoa maji machafu.
Wapevu wa usubi-nondo ni mbu wadogo ambao hawazidi urefu wa mm 5-6. Mwili, miguu na mabawa yao zimefunikwa kwa nywele nyingi ambazo (kwa madume) mara nyingi huwa na rangi na kusababisha ruwaza za rangi. Kwa kawaida macho yao yana umbo la figo na kuwa yameunganishika juu ya kichwa. Kila kimoja cha vipapasio kinajumuisha scape (pingili ya kwanza), pedicel (pingili ya pili) na flagellomere (pingili za mbele) 12-14. Mabawa yana umbo la duaradufu yenye vena 9-10 za mbele hadi nyuma na karibu hakuna vena za kushoto hadi kulia. Spishi za usubi-nondo mara nyingi huonekana sawa na zinatofautishwa tu kwa umbo la sehemu za uzazi za dume.[1]
Mabuu ya usubi-nondo wamegawanyika katika pingili zinazogawanyika na kila mgawanyiko ukiimarishika mgongoni[2]. Mabamba imara za mgongo zina nywele za kweli na za ziada ambazo ni muhimu kwa kutambua spishi[3]. Tofauti na nusufamilia nyingine za Psychodidae fumbatio huishia kwenye neli iliyo na spirakulo kadhaa nchani[2].
Spishi kadhaa za Afrika
[hariri | hariri chanzo]
|
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Psychoda alternata
-
Telmatoscopus sp.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Wagner, Rüdiger; Koç, Hasan; Özgül, Okan; Tonguç, Alper (2013). "New moth flies (Diptera: Psychodidae: Psychodinae) from Turkey". Zoology in the Middle East (kwa Kiingereza). 59 (2): 152–167. doi:10.1080/09397140.2013.810880. ISSN 0939-7140.
- ↑ 2.0 2.1 "Diptera | What Bug Is That?". anic.csiro.au. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-09-24. Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ Kvifte, G. M.; Wagner, R. (2017). "PSYCHODIDAE (Sand Flies, Moth Flies or Owl Flies)". Manual of Afrotropical Diptera. Volume 2. Nematocerous Diptera and lower Brachycera. South African National Biodiversity Institute. ISBN 9781928224129.