Peramiho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Peramiho
Peramiho is located in Tanzania
Peramiho
Peramiho
Mahali pa Peramiho katika Tanzania
Majiranukta: 10°38′8″S 35°27′44″E / 10.63556°S 35.46222°E / -10.63556; 35.46222
Nchi Tanzania
Mkoa Ruvuma
Wilaya Songea Vijijini
Idadi ya wakazi
 - 15,031
Peramiho

Peramiho ni kata ya Wilaya ya Songea Vijijini katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania. yenye postikodi namba 57213 .[1]

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,031 waishio humo. [2].

Abasia na parokia[hariri | hariri chanzo]

Inajulikana hasa kutokana na abasia ya wamonaki Wakatoliki Wabenedikto.

Abasia hiyo ilianzishwa kama kituo cha umisionari na P. Cassian Spiess O.S.B. aliyefika Peramiho mwaka 1898.

Mnamo mwaka 1931 Peramiho ilifanywa kuwa abasia na pia makao ya jimbo chini ya Abate-Askofu Gallus Steiger O.S.B..

Makao ya jimbo yalihamishiwa Songea mnamo mwaka 1969, na siku hizi kuna majimbo matatu (Jimbo kuu la Songea, Jimbo Katoliki la Njombe na Jimbo Katoliki la Mbinga) yaliyotokana na jimbo la zamani la Peramiho.

Peramiho kuna shule na hospitali nzuri pamoja na monasteri.

Pia ni makao makuu ya parokia ya Peramiho ambayo ina vigango vifuatavyo: Parangu, Lilambo, Likuyu, Mwanamonga, Litowa, Nakahuga, Sinai, Maposeni, Mdunduwalo na Morogoro.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/ruvuma.pdf
  2. Sensa ya 2012, Ruvuma - Songea District Council

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Pugu Hadi Peramiho - kimehaririwa na P. Gerold Rupper, OSB, BPNP, Peramiho 1988, ISBN 9967 67 031 1

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]