Peloponesi
Peloponesi (Kigiriki Πελοπόννησος peloponesos) ni rasi ya kusini mwa Ugiriki. Imeunganika na sehemu ya bara ya nchi kwa shingo la nchi kwenye mji wa Korintho.
Jina la kihistoria la rasi lilikuwa Morea (Μωριάς morias).
Eneo lote la Peloponesi ni kilomita za mraba 21,549. Kuna watu 1,155,000 walioishi huko mwaka 2011.
Peninsula imegawanywa kati ya mikoa mitatu ya kiutawala: sehemu kubwa ni ya mkoa wa Peloponesi, na sehemu ndogo ni za mkoa wa Ugiriki Magharibi na wa Attica.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Ghuba ya Korintho inatenganisha Peloponesi na Ugiriki bara.
Rasi hiyo ina milima mingi na pwani yenye hori ndefu zinazoingia ndani ya nchi. Mlima mrefu ni Taygetos unaofikia mita 2,407 juu ya UB. Rasi yote inakabiliwa na mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.
Mji mkubwa zaidi ni Patras yenye wakazi 170,000.
Miji
[hariri | hariri chanzo]Miji mikubwa zaidi ya kisasa kwenye Peloponesi ni (sensa ya 2011):
- Patras - wenyeji 170,896
- Kalamata - wenyeji 62,409
- Korintho - wenyeji 38,132
- Tripoli - wenyeji 30,912
- Aigio - wenyeji 26,523
- Pyrgos - wenyeji 25,180
- Argos - wenyeji 24,700
- Sparta - wenyeji 19,854
- Nafplio - wenyeji 18,910
Historia
[hariri | hariri chanzo]Rasi hii iliona vipindi na watendaji muhimu katika historia ya Ugiriki ya Kale.
- Ustaarabu wa Mikene ulistawi mnamo 1600 KK - 1100 KK ulikuwa eneo la maendeleo ya tekinolojia ya zama za bronzi katika Ulaya. Mikene ilikuwa mji kaskazini mwa Peloponesi.
- Tangu mwaka 776 KK Michezo ya Olimpiki ilifanyika Olimpia magharibi mwa Peloponesi.
- Miji mikubwa ya kale Sparta, Korintho, Argos na Megalopolis yote ilikuwa kwenye Peloponesi na kwa muda mrefu ilishirikiana katika Shirikisho la Peloponesi.
- Kwenye miaka 431 KK - 404 KK vita ya Peloponesi iliona mapigano makali kati ya Sparta na Atheni.
- Tangu mwaka 146 KK Peloponesi pamoja na Ugiriki yote ilikuja chini ya utawala wa Dola la Roma. Pamoja na sehemu nyingine za Roma ya Kale hata hapa watu wengi walipokea dini mpya ya Ukristo.
- Baada ya kuporomoka kwa Dola la Roma makabila ya Waslavi walianza kuhamia Peloponesi; baada ya karne kadhaa Waslavi hao walikuwa wameshapokea Ukristo na kutumia lugha ya Kigiriki[1]
- Katika karne ya 15 Milki ya Osmani ilianza kuvamia Ugiriki na hadi mwaka 1532 hivi Ugiriki yote pamoja na Peloponesi ilikuwa chini ya Milki ya Osmani.[2]
- Mwaka 1821 Vita ya Uhuru wa Ugiriki ilianza Kalamata kwenye Peloponesi [3] ikaendelea hadi kutambuliwa kwa Ugiriki kuwa nchi huru mnamo 1830.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Stamatoyannopoulos, George et al., Genetics of the Peloponnesian populations and the theory of extinction of the medieval Peloponnesian Greeks, European Journal of Human Genetics, 25.5 (2017), pp. 637–645
- ↑ Bées & Savvides (1993), p. 239
- ↑ Richard Clogg (20 Juni 2002). A Concise History of Greece. Cambridge University Press. ku. 35–42. ISBN 978-0-521-00479-4.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Peloponesi travel guide kutoka Wikisafiri
- Britannica.com
- Official Regional Government Website
- Greek Fire Survivors Mourn Amid Devastation in Peloponnese.
- Stewart, Daniel (2013). "Storing up Problems: Labour, Storage, and the Rural Peloponnese". Internet Archaeology (34). doi:10.11141/ia.34.4.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Peloponesi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |