Pelegrino Laziosi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya uponyaji wake.

Pelegrino Laziosi, O.S.M. (Forlì, Italia, 1260 hivi - Forlì, Italia 1 Mei 1345) alikuwa padri mtawa wa shirika la Watumishi wa Maria[1].

Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri mwaka 1609, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1726.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 1 Mei[2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa familia iliyomuunga mkono kaisari dhidi ya Papa, alimdharau na labda kumpiga Filipo Benizi, mkuu wa Watumishi wa Maria aliyekuwa ametumwa na Papa mjini Forlì. Baadaye kidogo, alikwenda kumuomba msamaha, na miaka kumi baadaye akajiunga la shirika lake akapadrishwa.

Alitumwa Forlì kuanzisha nyumba ya shirika akapendwa na umati kwa mahubiri na maadili yake, pamoja na miujiza iliyomfanya ateuliwe kuwa msimamizi wa wagonjwa wa saratani.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.